Tetesi za soka Ulaya, Jumatano Julai 12 2023

Joel JJ By Joel JJ β€’ 12th July 2023


Tetesi za soka Ulaya, Jumatano Julai 12 2023

Kiungo wa kati wa Juventus na Ufaransa Paul Pogba, 30, atapewa ofa ya pauni milioni 128 kwa miaka mitatu ili kujiunga na klabu moja nchini Saudi Arabia. (Gazzetta dello Sport)

Mshambuliaji wa Tottenham na England Harry Kane anataka kujiunga na Bayern Munich msimu huu wa joto huku mabingwa hao wa Bundesliga wakifikiria kuwasilishaofa ya tatu kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29. (ESPN)

Bournemouth wako mbele ya Tottenham, West Ham na Wolves katika harakati za kumsaka kiungo wa Bristol City Muingereza Alex Scott, 19. (Teamtalk)

Viktor Gyokeres anatazamiwa kuondoka Coventry kwenda Sporting Lisbon katika siku zijazo huku klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ikitarajia ada inayoweza kufikia £20.5m kwa ajili ya mshambuliaji huyo wa Sweden mwenye umri wa miaka 25. (Mail)

Chelsea wanajiandaa kupeleka ofa yakwanza kwa mshambuliaji wa Lyon Mfaransa Rayan Cherki, 19. (ESPN)

Everton wanavutiwa na mshambuliaji wa Manchester United na Sweden Anthony Elanga, 21. (Foot Mercato)

Burnley wamemfanya kiungo wa kati wa Coventry Mholanzi mzaliwa wa Brazil Gustavo Hamer, 26, kuwa chaguao lao linalofuata. (Telegraph)

Manchester United wanakaribia kufikia makubaliano ya kumnasa mlinda mlango wa Inter Milan na Cameroon Andre Onana, 27. (Sky Sports)

Nottingham Forest wako kwenye mazungumzo na Manchester United kuhusu mpango wa kumnunua mlinda mlango wa England Dean Henderson, 26, na pia wanafikiria kumnunua kipa wa Wolves Mreno Jose Sa, 30. (Telegraph)

Arsenal wana matumaini ya kukamilisha usajili wa kiungo wa kati wa West Ham na England Declan Rice, 24, kabla ya kikosi hicho kuruka kuelekea Marekani kwa ziara yao ya kujiandaa na msimu ujao Jumapili. (Sky Sports)

Southampton wanafikiria kumnunua winga wa Hoffenheim na Denmark Jacob Bruun Larsen, 24. (Mail)

Arsenal wameungana na Tottenham na Chelsea katika kinyang'anyiro cha kumnunua kiungo wa kati wa Celta Vigo raia wa Hispania Gabri Veiga, 21 - lakini Paris St-Germain hawana mpango. (Le10Sport)

Manchester City wanakaribia kumsajili beki wa kati wa Manchester United mwenye umri wa miaka 16, Harrison Parker ili 'kulipiza kisasi' kwa United kujaribu kuwasajili mapacha wao Jack na Tyler Fletcher wenye umri wa miaka 16. (Manchester Evening News)

BBC


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.