Klabu ya Simba leo imeingia makubaliano ya Ushirikiano na Bank ya CRDB katika kusajili Mashabiki wa klabu ya Simba
Akizungumza katika hafla iliyofanyika viwanja vya Leaders leo, Mtendaji Mkuu wa Simba Iman Kajula, amesema Simba inatarajiwa kutoa kadi za aina tatu ambazo zote zitapatikana katika Matawi yote ya CRDB nchi nzima
"Katika ushirikiano wetu na CRDB tutakua kadi za aina tatu, kadi za watoto chini ya umri wa miaka 18, kadi za mashabiki wa kawaida na kadi za Platinum. Kadi zote zitakua ni Visa ambayo mtu anaweza kufanya miamala popote duniani," alisema Kajula
Aidha kampuni yua CRDB imeanzisha akaunti maalum kwa ajili ya mashabiki wa Simba, akaunti ambayo kwa atakayekuwa nayo atapata bima yenye thamani ya Tsh Milioni 2
Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Abdul Majid Nsekela amesema pia wameanzisha akaunti kwa ajili ya kina Mama itakayoitwa Simba Queens Account
"Tumeanzisha Simba Account, Maalumu kwa ajili ya mashabiki wetu, pia tumeanzisha Account kwa ajili ya kina Mama itakayoitwa Simba Queens Account (Account ya Malkia wa Simba) Shabiki wa Simba akiwa na Account hizi atapata Bima yenye thamani ya Shilingi milioni 2," alisema
Viongozi na wadau mbalimbali wa klabu ya Simba walihudhuria hafla hiyo ambayo imefungua ukurasa wa ushirikiano katika ya klabu ya Simba na CRDB
Simba inaarajiwa kufanya tukio la aina hiyo na benki ya NMB


