Yanga - Local

CRDB, Yanga kushirikiana Wiki ya Mwananchi

Joel JJ By Joel JJ
β€’
13 Jul 2023
CRDB, Yanga kushirikiana Wiki ya Mwananchi

Benki ya CRDB imeingia makubaliano na klabu ya Yanga kudhamini Wiki ya Mwananchi ambayo imeanza rasmi leo na kilele chake kikiwa Julai 22 pale uwanja wa Benjamin Mkapa

Mtendaji Mkuu wa Yanga Andre Mtine amesema wanafurahi kushirikiana na CRDB katika tukio hili kubwa linaloambatana na matukio ya kijamii na burudani

"Tunayo furaha kushirikiana na CRDB katika tukio kubwa la Wiki ya Mwananchi ambalo tutalihitimisha uwanja wa Benjamin Mkapa Julai 22 kwa mchezo wa Kimataifa wa kirafiki dhidi ya Kaizer Chiefs"

"Mashabiki wetu watapata burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali pamoja na mchezo huu utakaozikutanisha timu zenye historia kubwa barani Afrika"

Naye Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema mashabiki wa Yanga wajiandae kwa Wiki ya Mwananchi ya kihistoria kwani wameandaa burudani ya aina yake

Kamwe amesema mashabiki watapata nafasi ya kuwashuhudia wachezaji wapya katika mechi kubwa dhidi ya Kaizer Chiefs akiamini mchezo huo utaonyesha ubora wa wachezaji hao

"Tumeileta Kaizer Chiefs ambayo ina wachezaji bora kama tulivyo sisi, tunaamini mchezo huu utakuwa kipimo sahihi kwa wachezaji wetu tuliowasajili"

"Sisi hatuleti timu dhaifu ili kuwaaminisha mashabiki kuwa timu yetu ni bora na kusababisha vilio pale ligi inapoanza," alisema Kamwe

Kamwe amesema wanaendelea kutambulisha wachezaji siku ya leo na kesho ambapo utambulisho huo utahitimishwa mwanzoni mwa wiki ijayo kwa kumtambulisha mchezaji jezi namba sita

Wiki ya Mwananchi HII IMEENDAA itazinduliwa rasmi Jijini Mwanza Jumamosi ya tarehe 15 Julai 2023 na kutakuwa na matukio mbalimbali ya kijamii na burudani ya kutosha kwa wananchi Mwanza katika viwanja vya Furahisha

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
6h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
6h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
7h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
10h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
14h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
14h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
15h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
16h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
16h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
17h ago
READ MORE β†’