Singida - Local

Pluijm aongeza mwaka Singida FG

Joel JJ By Joel JJ
β€’
16 Jul 2023
Pluijm aongeza mwaka Singida FG

Uongozi wa Singida Fountain Gate iliyopo Ligi Kuu Bara na itakayoshiriki michuano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho Afrika, umemuongezea mkataba wa mwaka mmoja kocha mkuu wa timu hiyo Mholanzi Hans Pluijm

Pluijm aliyeiwezesha timu hiyo kumaliza nafasi ya nne na kufuzu michuano ya CAF msimu ujao, alimaliza mkataba na klabu hiyo tangu Juni 30, mwaka huu jambo lililozua hofu juu ya hatima yake ndani ya kikosi hicho

Pluijm amesema amejisikia furaha kupewa mkataba huo huku akiahidi mambo makubwa msimu ujao licha ya kukiri ushindani utakuwa ni mkubwa kutokana na mashindano mbalimbali ambayo timu hiyo itakuwa ikishiriki

"Msimu wa kwanza ulikuwa ni mzuri kwetu kwa sababu tuliweza kufikia malengo tuliyojiwekea lakini bado tuna kazi kubwa ya kufanya hivyo kitendo cha kuongezewa mkataba ni ishara tosha viongozi wangu wananiamini ingawa kwangu ni deni,"alisema

Kwa upande wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa timu hiyo, Olebile Sikwane amesema;

"Pluijm alianza na timu hivyo hatukuhitaji kufanya maboresho kwenye idara hiyo, tuna matumaini makubwa kwake na kama ambavyo nilisema tangu nimeteuliwa kwenye nafasi hii malengo yetu ni kuleta ushindani kwenye mashindano ya ndani na nje"

Mwanaspoti

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
29m ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
41m ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
1h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
4h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
8h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
8h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
9h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
10h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
10h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
11h ago
READ MORE β†’