Mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele atajiunga na Pyramids Fc ya Misri baada ya makubaliano kufikiwa, imefahamika
Mayele alishafikia makubaliano binafsi ya Pyramids wiki kadhaa zilizopita, timu hiyo imekamilisha mazungumzo na Yanga baada ya kukubaliana ada ya uhamisho
Katika uhamisho wa Mayele kwenda Pyramids Yanga inatarajiwa kuvuna takribani Tsh Bil 2.8 na kumfanya Mayele kuwa mchezaji ghali zaidi kuwahi kununua timu za Tanzania akimpiku Luis Miquissone ambaye usajili wake kutoka Simba kwenda Al Ahly uliingizia Simba Tsh Bilioni 2
Pamoja na kuwa bado Yanga hawajatangaza taarifa rasmi kuhusu Mayele kuondoka, lakini ni suala la muda tu kwani wako kwenye mchakato wa kusajili mshambuliaji mwingine kuziba nafasi yake
Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema timu hiyo inatarajiwa kutangaza usajili wa wachezaji wanne wiki hii ambapo mmoja ni usajili wa ndani na watatu ni nyota wa kigeni
Miongoni mwa wachezaji hao, wawili watakuwa washambuliaji