Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Jumatano Julai 19 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
19 Jul 2023
Tetesi za soka Ulaya, Jumatano Julai 19 2023

Chelsea wanafikiria kumnunua beki wa Manchester United na England Harry Maguire, 30. Beki wa The Blues Mfaransa Wesley Fofana, 22, huenda akasalia nje ya uwanja kwa muda mrefu baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti . (90 min)

Newcastle United wanaweza kukamilisha dili la kumnunua winga wa Leicester City na Uingereza Harvey Barnes siku chache zijazo na kuwasili kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kunaweza kumaanisha mshambuliaji wa Ufaransa Allan Saint-Maximin kuondoka Magpies. Saudi Pro League. (Mail)

Al-Ahli wanamtaka Saint-Maximin na wameipatia Newcastle ofa ya euro milioni 25 kwa ajili ya mchezaji huyo. (L'Equipe - kwa Kifaransa)

Klabu ya Saudi Arabia, Al-Hilal inavutiwa na mshambuliaji wa Liverpool Luis Diaz lakini kuna uwezekano kuwa Reds watakubali euro 50m wanazotayarisha kutoa kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Colombia, 26. (Record - kwa Kireno)

Rais wa Paris St-Germain Nasser Al-Khelaifi alimuona Kylian Mbappe kwenye uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo Jumanne lakini aliamua kutofanya mazungumzo ya ana kwa ana na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 kama mzozo kati ya klabu hiyo ya Ligue 1 na mshambuliaji wa Ufaransa. iliendelea. (Sky Sports)

Aston Villa wameweka dau lililoboreshwa la hadi £42.9m kumnunua winga wa Bayer Leverkusen na Ufaransa Moussa Diaby. (Athletic- Usajili unahitajika)

Manchester United itawasilisha ombi la kumnunua mshambuliaji wa Atalanta na Denmark Rasmus Hojlund, 20, lakini klabu hiyo ya Italia itakataa euro milion 70, Uited wako iko tayari kuelekeza mawazo yao kwa mshambuliaji wa Eintracht Frankfurt Mfaransa Randal Kolo Muani. 24. (ESPN)

Marseille wanajiandaa kufanya mazungumzo na Chelsea kuhusu Pierre-Emerick Aubameyang, baada ya kufikia mkataba wa miaka mitatu na mshambuliaji huyo wa Gabon mwenye umri wa miaka 34. (Guardian)

Chelsea wanataka zaidi ya pauni milioni 40 kwa Connor Gallagher, 23, huku West Ham wakipania kumleta kiungo huyo wa kati wa Uingereza katika Uwanja wa London Stadium. (Sky Sports)

Bayern Munich wako tayari kumuuza kiungo wa kati wa Ujerumani Joshua Kimmich wakipokea ofa sahihi kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28. (Kicker - kwa Kijerumani)

Beki wa Manchester United Alex Telles anakaribia kuhamia klabu ya Saudi Arabia Al-Nassr, huku klabu zote mbili zikizungumza kuhusu Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 30. (Athaletic-Usajili unahitajika)

Tottenham wanajadiliana na klabu ya Italia Napoli kuhusu uwezekano wa kuuzwa kwa kiungo wa Argentina Giovanni Lo Celso, 27. (Redio Punto Nuovo kupitia Football Italia)

BBC

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
32m ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
45m ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
1h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
4h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
8h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
8h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
9h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
10h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
10h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
11h ago
READ MORE β†’