Kocha Yanga matumaini kibao

Joel JJ By Joel JJ β€’ 21st July 2023


Kocha Yanga matumaini kibao

Baada ya kukinoa kikosi kwa takribani wiki moja, Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema ana imani atakuwa na wakati mzuri na mabingwa hao wa nchi

Gamondi amesema kwa muda mchache aliokaa na kikosi chake amewaona wachezaji wanavyojituma na kujitambua kitu ambacho kinampa imani ya kufanya vizuri

"Nimezoea kufanya kazi katika shinikizo hasa katika soka la Afrika, mashabiki wanahitaji matokeo muda wote kwa hiyo ni lazima ukiwa kocha ujue kuishi katika nyakati zote ukiwa umeshinda au umepoteza"

"Ndio kwanza tumeanza maandalizi ya msimu lakini mpaka sasa tunakwenda vizuri, wachezaji wana ari na morali ya kupambana hili jambo zuri," alisema Gamondi

Gamondi amesema yeye pamoja na benchi lake la ufundi wanafahamu kazi kubwa iliyo mbele yao kwani wamekabidhiwa timu ambayo imetoka kupata mafanikio makubwa

Kocha huyo ameongeza kwa kusema kuwa anavutiwa na mazingira ya Tanzania hasa utamaduni wa mashabiki wa soka nchini kujitokeza kwenye matukio mbalimbali yanayohusu timu zao


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.