Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Jumamosi Julai 22 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
22 Jul 2023
Tetesi za soka Ulaya, Jumamosi Julai 22 2023

Mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich wanavutiwa na kiungo wa kati wa Liverpool na Brazil Fabinho, 29, ikiwa uhamisho wake wa kwenda Al-Ittihad hautafanikiwa. (Sky Germany)

Bayern wanapanga kutoa ofa ya tatu kwa mshambuliaji wa Tottenham na England Harry Kane na wana uhakika wa kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29. (Times)

Atalanta hawako tayari kuacha hesabu yao ya pauni milioni 86 kwa mshambuliaji wa Denmark Rasmus Hojlund, 20, ambaye analengwa zaidi na Manchester United.(Mail)

Paris St-Germain pia wanavutiwa na Hojlund na wameanza majadiliano. (L'Equipe )

Fiorentina wanasema bado hawajapokea ofa rasmi kutoka kwa Manchester United kwa kiungo wa Morocco Sofyan Amrabat, 26. (Metro)

Mlinzi wa Uingereza Kyle Walker, 33, anatamani kuzungumza na Bayern Munich anapofikiria kuondoka Manchester City msimu huu wa joto. (Sky Sports)

Crystal Palace wana imani kuwa mshambuliaji wa Ivory Coast Wilfried Zaha, 30, atasaini mkataba mpya licha ya kutakiwa na Al-Ettifaq na Lazio. (Telegraph)

Manchester City wanamshinikiza kiungo wa kati wa Ureno Bernardo Silva, 28, kujibu kuhusu ofa yao mpya ya mkataba wa pauni 300,000 kwa wiki. (Mirror)

Nottingham Forest inajaribu kusajili wachezaji wawili kutoka Manchester United, winga wa Uswidi Anthony Elanga, 21, kwa mkataba wa kudumu na mlinda lango wa Uingereza Dean Henderson, 26, kwa mkopo. (Fabrizio Romano)

Atletico Madrid wanajiandaa kushindana na Chelsea kumnunua mshambuliaji wa Montpellier Mfaransa Elye Wahi, 20. (Express)

Wahi anasema hataki kwenda kwa klabu dada ya Chelsea Strasbourg kwa mkopo iwapo The Blues watamsajili. (Mercato)

Mlinzi wa kushoto wa Brazil Alex Telles, 30, yuko mbioni kukamilisha uhamisho wake wa £4m kutoka Manchester United kwenda Al-Nassr.(Mirror). Nottingham Forest pia wanakaribia kumsaini mchezaji huru Ola Aina, 26, baada ya mkataba wa beki huyo wa Nigeria kukamilika Torino.(Nottingham Post)

Beki wa kulia wa Southampton England chini ya umri wa miaka 21 Tino Livramento, 20, anakaribia kuhamia Newcastle. (Chronicle Live)

Liverpool, Paris St-Germain na Atletico Madrid wanavutiwa na kiungo wa kati wa Mali Cheick Doucoure, 23, lakini Crystal Palace wanadai pauni milioni 65. (90min)

Liverpool wanafanya mazungumzo na Preston North End kuhusu kuuzwa kwa mshambuliaji wa Uingereza Layton Stewart, 20. (Liverpool Echo)

Kiungo wa kati wa Uhispania Thiago, 32, anafikiria kuhama Liverpool na kuhamia Uhispania, Saudi Arabia na Uturuki. (Diario Sport )

Beki wa Uholanzi Ki-Jana Hoever, 21, na winga wa Ureno Chiquinho, 23, wako kwenye hatihati ya kujiunga na Stoke kwa mkopo msimu huu kutoka Wolves. (Express na Star)

Beki wa Fiorentina Mbrazil Igor, 25, anatazamiwa kukamilisha uchunguzi wa kimatibabu huko Brighton Jumatatu baada ya vilabu hivyo kukubaliana juu ya ada ya £14.7m (euro 17m)(Fabrizio Romano)

Maombi mawili ya Monaco yamekataliwa kwa mlinzi wa Southampton na Ghana Mohammed Salisu, 24, na huenda wakasubiri hadi Januari watakapoweza kujadili uhamisho wa bila malipo. (Mail)

BBC

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
3h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
3h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
4h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
7h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
11h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
11h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
12h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
12h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
13h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
14h ago
READ MORE β†’