Chelsea na klabu ya Saudia Al-Hilal zimeanza mchakato wa kujaribu kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 24, ambaye hajasafiri na Paris St-Germain katika ziara yao ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi huko barani Asia. (RMC Sport)
Al-Hilal wamempa Mbappe ofa ile ile waliyotoa kwa Lionel Messi - euro 400m (£346.3m) kwa mwaka hadi 2026, ingawa kimsingi ana makubaliano ya kujiunga na Real Madrid kama mchezaji huru msimu ujao wa joto. (Nicolo Schira)
Mbappe yuko tayari kukaa nje kwa msimu mzima na kuondoka PSG bure msimu ujao baada ya mabingwa hao wa Ufaransa kumuweka sokoni Ijumaa. (Sky Sports)
Mkewe Harry Kane, 29 ameonekana mjini Munich, akitafuta nyumba na shule kabla ya uwezekano wa nyota huyo kuhama kutoka Tottenham kwenda Bayern Munich. (Bild)
Chelsea imefanya mawasiliano na Ajax kuhusu nia yao ya kutaka kumsajili kiungo mshambuliaji wa Ghana Mohammed Kudus, 22. (The Athletic)
Mazungumzo ya mkataba mpya kati ya Victor Osimhen na timu yake ya Napoli bado yamekwama, na hivyo kufungua milango kwa Chelsea au Manchester United kujaribu kumsajili mshambuliaji huyo wa Nigeria, 24. (Corriere dello Sport, via Goal)
Inter Milan wanaamini kuwa sasa haiwezekani kufikiria kumrejesha Romelu Lukaku katika klabu hiyo kutoka Chelsea baada ya mshambuliaji huyo wa Ubelgiji, 30, kuwasiliana na wapinzani wao AC Milan na Juventus kuhusu uwezekano wa kuhamia huko. (Gazzetta dello Sport)
Galatasaray wamempa ofa yenye thamani ya £8m kwa mwaka mshambuliaji wa Ivory Coast Wilfried Zaha, 30, ambaye ni mchezaji huru baada ya mkataba wake pale Crystal Palace kumalizika. (Barua Jumapili)
Mshambuliaji wa Uruguay Luis Suarez, 36, yuko tayari kulipa kutoka mfukoni mwake ili kuondoka Gremio na kwenda klabu ya Inter Miami, kuungana tena na mchezaji mwenzake wa zamani wa Barcelona Lionel Messi (ESPN, via Sport)
Manchester City wameambiwa watalazimika kulipa thamani pesa pauni milioni 87 kwenda RB Leipzig ili kumsajili mlinzi wa Croatia Josko Gvardiol, 21. (Sunday Mirror). Crystal Palace wanafikiria kumnunua mlinzi wa Manchester City ambaye hajatulia Aymeric Laporte, 29. (Star Sunday)
Manchester United wanaonekana kuwa tayari kumuongeza mkataba wa mwaka wa ziada beki wa kulia wa England Aaron Wan-Bissaka, 25, kama kipengele cha mkataba wake kinavyoruhu, licha ya Palace kutaka kumsajili tena. (Star Sunday)
Fulham wanatazamiwa kutumia zaidi ya £30m kununua mabeki wawili wapya wa kati - Mchezaji wa kimataifa wa Ghana wa Southampton Mohammed Salisu, 24, na mlinzi wa Ajax mzaliwa wa Italia na Nigeria Calvin Bassey, 23. (Sunday Telegraph)
Mshambulizi wa Jamaica Michail Antonio, 33, ana nia ya kuhama West Ham ili kujiunga na Al-Ettifaq ya Steven Gerrard msimu huu wa joto. (Football Insider)
BBC