Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Jumatatu Julai 24 2023

Joel JJ By Joel JJ
24 Jul 2023
Tetesi za soka Ulaya, Jumatatu Julai 24 2023

Mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy ameambiwa lazima amuuze Harry Kane msimu huu wa joto ikiwa hawezi kumshawishi mshambuliaji huyo wa England, 29, kusaini mkataba mpya. (Telegraph)

Taarifa za uamuzi wa Tottenham zimeiweka tena mguu sawa Manchester United juu ya kumsajili Kane. (Mirror)

Bayern Munich tayari imekataliwa ofa zake mbili za kutaka kumnunua Kane na sasa wanatayarisha ofa ya tatu. (Mail) Bayern wako tayari kumpa Kane mkataba wa muda mrefu wa miaka minne, ikiwezekana mitano. (Bild)

Chelsea wamewasilisha ofa kwa mchezaji wa Crystal Palace Michael Olise na winga huyo wa Ufaransa, 21, tayari ana makubaliano ya awali na The Blues. (RMC Sport)

Manchester City pia wana nia ya kumsajili nyota huyo wa Ufaransa chini ya umri wa miaka 21 Olise, ambaye ana kipengele katiba mkataba wake cha kuuzwa kwa takriban £35m. (Fabrizio Romano)

Al-Hilal itaweka dau la euro 200m (£173m) kwa ajili ya Kylian Mbappe wa Paris St-Germain na kumpa mshambuliaji huyo wa Ufaransa, 24, kandarasi ya miaka miwili yenye thamani ya euro 200m kwa mwaka, ikiwezekana na kipengele cha kuuzwa baada ya mwaka mmoja pekee ili kuhamia Real Madrid. (Tancredi Palmeri)

Chelsea wanachoshwa na kuishiwa uvumilivu na Romalu Lukaku, kutokana na mshambuliaji huyo wa Ubelgiji, 30, kugoma kuhamia Saudi Arabia na anasubiri klabu ya Ulaya kumsajili. (Gazzetta dello Sport)

Uhamisho wa Fabinho kutoka Liverpool kwenda Al-Ittihad uko hatarini a kwani kiungo huyo wa kati wa Brazil, 29, anataka ufafanuzi iwapo anaweza kwenda na mbwa wake wawili huko Saudi Arabia. (Express)

Mshambulizi wa Atalanta na Denmark Rasmus Hojlund, 20, anataka kukamilisha uhamisho wa kwenda Manchester United kufikia mwisho wa mwezi akiwa tayari amekubali masharti ya kibinafsi. (TeamTalk)

Mshambuliaji wa Ivory Coast Wilfried Zaha, 30, atajiunga na mabingwa wa Uturuki Galatasaray bure baada ya kumaliza kataba wake Crystal Palace. (Guardian)

Meneja Marco Silva amekataa ofa ya pauni milioni 40 kutoka kwa klabu ya Al-Ahli ya Saudi Arabia na kuamua kusalia Fulham. (Telegraph)

Chelsea wameanzisha tena mazungumzo na timu zake Saudi Arabia kuhusu kumuuza winga wa Morocco Hakim Ziyech, 30. (Teamtalk)

Winga wa Uingereza Callum Hudson-Odoi, 22, anakaribia kuungana tena na kocha wake wa zamani wa Chelsea Maurizio Sarri huko Lazio. (Gazzetta dello Sport)

Hata hivyo, Fulham bado wanajaribu kuipiku Lazio katika kumsajili Hudson-Odoi kutoka Chelsea. (Nicolo Schira) Fulham wako tayari kulipa pauni milioni 7 kwa Demarai Gray huku Everton wakitafuta pesa kumnunua winga huyo wa Jamaica, 27. (Sun)

West Ham wana uhakika wa kukamilisha dili la kumnunua kiungo wa kati wa Mexico Edson Alvarez, 25, kutoka Ajax kwa ada ya £40m msimu huu. (Football Insider)

Atletico Madrid wamewasiliana na Paris St-Germain kuhusu kumsajili kiungo wa kati wa Italia Marco Verratti, 30, lakini Liverpool pia wanavutiwa nae, huku kiungo wa Tottenham Mdenmark Pierre-Emile Hojbjerg, 27, akiwa ni mmoja wa mbadala wa Atletico. (Marca)

Fulham wamekataa dau la pauni milioni 50 kutoka kwa West Ham kumnunua kiungo wa kati wa Ureno Joao Palhinha, 28. (90min)

Mshambulizi wa Italia Gianluca Scamacca, 24, anaweza kujiunga na Roma ikiwa West Ham itamsajili mshambuliaji wa Ubelgiji Divock Origi, 28, kutoka AC Milan, baada ya mazungumzo na Chelsea kuhusu mshambuliaji wa Albania Armando Broja, 21, kuvunjika. (Gazetta dello Sport)

Baada ya kuondoka Liverpool kutokana na kumalizika kwa kandarasi yake, kiungo wa zamani wa Uingereza Alex Oxlade-Chamberlain, 29, anavivutia vilabu vya Saudi Arabia, Besiktas na Brentford. (Mirror)

BBC

More Stories

BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
53m ago
READ MORE →
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
1h ago
READ MORE →
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
2h ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
2h ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
2h ago
READ MORE →
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
2h ago
READ MORE →
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
3h ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
4h ago
READ MORE →
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
15h ago
READ MORE →
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
15h ago
READ MORE →