Klabu ya Simba imethibitisha kumuuza winga Pape Ousmane Sakho klabu ya Quevilly Rouen Metropole ya nchini Ufaransa
Sakho hakuwa sehemu ya kikosi kilichosafiri na Simba kwenye pre-season Uturuki akisubiri kukamilika kwa uhamisho wake
Juzi Simba ilitangaza kumrejesha winga Luis Miquissone na jana kutangaza kusajili mlinda lango Jefferson kutoka Brazil
Usajili wa wachezaji hao ulipelekea timu hiyo kuwa na nyota 14 wa kigeni na hivyo kulazimika kuachana na wachezaji wawili
Mchezaji mwingine anayetarajiwa kuachwa na Simba ni Peter Banda ambaye huenda akatolewa kwa mkopo



