Tetesi za soka Ulaya, Jumatano Julai 26 2023

Joel JJ By Joel JJ β€’ 26th July 2023


Tetesi za soka Ulaya, Jumatano Julai 26 2023

Uhakika wa Bayern Munich wa kumsajili mshambuliaji wa England Harry Kane kutoka Tottenham Hotspur unazidi kuongezeka na hawajali kuhusu taarifa za kwamba Paris St-Germain pia wanamtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29. (Sky Sports)

Mtendaji mkuu wa Bayern Jan-Christian Dreesen na Mkurugenzi wa ufundi Marco Neppe wamebaki Ujerumani, badala ya kujiunga na timu kwenye kambi ya huko Japan, ili kukamilisha mpango wa pauni milioni 100 kwa ajili ya kumsajili Kane. (Mirror)

PSG inatarajia kupokea ofa ya pesa pamoja na mchezaji kutoka vilabu vya Ulaya ili kumuuza Kylian Mbappe, baada ya kupokea ofa ya rekodi ya dunia ya £259m kutoka kwa Al-Hilal

Chelsea, Manchester United, Tottenham, Inter Milan na Barcelona zimeonyesha nia ya kumuhitaji mshambuliaji huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 24. . (Press Association, via Independent)

Kipa wa Urawa Red Diamonds na Japan Zion Suzuki, 20, amekataa kuhamia Manchester United. (Sponichi)

Manchester City wamemwambia kiungo wa kati wa Ureno Bernardo Silva kuwa hawana nia ya kumuuza msimu huu wa joto licha ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 kutaka kuondoka. (90Min)

West Ham wamefanya mazungumzo ya awali na Manchester United kuhusu kumsajili beki wa England Harry Maguire, 30, na kiungo wa kati wa Scotland Scott McTominay, 26. (Sky Sports)

Lakini West Ham wamekatishwa tamaa na bei ya £40m wanayoitaka Manchester United kwa ajili ya McTominay. (Mirror)

Ombi la The Hammers au wapiga nyundo hao wa London la kumnunua kiungo wa Chelsea Conor Gallagher, 23, limekataliwa lakini wana imani kuwa wanaweza kuipiku Tottenham kupata saini ya mchezaji huyo wa kimataifa wa England. (Standard)

Southampton wamekataa ofa inayodhaniwa kuwa ya thamani ya pauni milioni 35 kutoka Liverpool kwa ajili ya kiungo wa kati raia wa Ubelgiji Romeo Lavia, 19, huku klabu hiyo ya Pwani ya Kusini ikitaka angalau pauni milioni 50. (Guardian)

Uhamisho wa kiungo wa kati wa Liverpool na Brazil Fabinho kwenda Al-Ittihad ya Saudi Arabia uko hatarini kuvunjika huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 akitarajiwa kuanza tena maandalizi ya msimu mpya akiwa na wekundu hao wa Anfield. (The Athletic)

Kiungo wa kati wa Ujerumani Joshua Kimmich anatarajiwa kusalia Bayern Munich baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 kusema kwamba "ana uhakika" wa kupata muda mwingi wa kucheza kwenye kikosi cha kwanza cha klabu hiyo ya Bundesliga katika msimu unaokuja. (Sky Germany)

Leeds United wanataka kumwongeza kipa Muingereza Karl Darlow kwenye kikosi chao na wanaonekana kupiga hatua katika jitihada zao za kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 kutoka Newcastle United. (TheAthletic)

Arsenal wanakaribia kumsaini kiungo wa kati wa Gremio na Brazil Bitello, 23, ambaye alikuwa anahusishwa na uhamisho wa kuelekea vilabu vya Serie A. (Tuttomercatoweb)

Mshambulizi wa Mali, El Bilal Toure, 21, ameamua kujiunga na Atalanta kutoka Almeria badala ya Everton iliyokuwa inamuhitaji pia. (L'Equipe)

Everton wako kwenye mazungumzo ya kumsajili mshambuliaji wa Italia Wilfried Gnonto, 19, kutoka Leeds United. (Football Insider)

BBC


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.