Klabu ya Azam FC imekamilisha uhamisho wa mchezaji wao Issah Ndala kwenda KMC FC kwa mkopo wa msimu wa mwaka mmoja.
Hii inakuja baada ya Azam FC kumuongeza kiungo kutoka Yanga Yanick Bangala na kufikia idadi ya wachezaji 13 wa kigeni kinyume na kanuni za Ligi Kuu zinazoagiza kila timu kuwa na wachezaji 12 tu wa kigeni
Ndala alijiunga na Azam FC msimu wa 2022/2023 kwa miaka mitatu na hakuwa na msimu mzuri kwa matajiri hao wa Chamazi baada ya majeraha kumuandama
Nyota huyo alitua Azam Fc akitokea klabu ya Plateu United, waliokuwa mabingwa wa ligi kuu ya Nigeria
Anakuwa mchezaji wa pili kutua KMC akitokea Azam Fc baada ya Pepsie Evans ambaye pia KMC walimsajili kwa mkopo wa msimu mzima
ADVERTISE HERE