Parma - Juventus - International

Buffon astaafu soka

Joel JJ By Joel JJ
β€’
2 Aug 2023
Buffon astaafu soka

Golikipa mkongwe raia wa Italia, Gianluigi Buffon amestaafu soka.  Buffon, 45, alikuwa akiitumikia Parma msimu uliopita

Muitaliano huyo alianza kuitumia klabu ya Parma mwaka 1995, ambapo mwaka 2001 aliachana na timu hiyo na kujiunga na Juventus zote za nchini Italia

Mwaka 2018 aliondoka na kujiunga na Paris Saint Germain, alidumu hapo kwa msimu mmoja na mwaka 2019 akarejea Juventus, baada ya kucheza mechi 17, mbele ya kipa Wojciech Szczesny mwaka 2021 akajiunga na Parma

Mafanikio makubwa ambayo Buffon ameyapata katika maisha yake ya soka ni kushinda Kombe la Dunia mwaka 2006 akiwa na Taifa la Italia, baada ya kuwafunga Ufaransa kwa mikwaju ya penalti

Lakini pia amewahi kushinda taji la Ligi Kuu Italia maarufu 'Seria A' mara 10, na kuchukuwa tuzo ya kipa bora mara 13

Buffon aliwahi kushinda tuzo ya kipa bora wa UEFA na mchezaji bora ngazi ya klabu mwaka 2002/2023

Amewahi pia kuchukua tuzo ya kipa bora Ulaya mwaka 2003, 2016, 2017. Lakini pia kipa bora wa Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2016/2017

Akiwa na PSG amewahi kushinda ubingwa wa Ligue 1 mwaka 2018/2019.

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
9h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
9h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
9h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
13h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
16h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
17h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
17h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
18h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
19h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
20h ago
READ MORE β†’