Klabu ya Simba imetangaza kuuza tiketi zote za Tamasha la Simba Day siku tatu kabla ya Tamasha lenyewe
Zoezi la manunuzi ya tiketi limefungwa rasmi, kwa wale ambao hawajakata tiketi mpaka sasa wameaswa wasuburi kushuhudia Tamasha hilo kupitia Azam TV
Simba Day itafanyika Jumapili, August 06 ambapo klabu ya Simba inatarajiwa kutambulisha kikosi chake kuelekea msimu wa 2023/24
Simba pia itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Power Dynamos ya Zambia
