Bayern Munich wanataka kuwasilisha ofa mpya ya euro 110m (£94.6m) kwa ajjili ya mshambuliaji wa Tottenham na England Harry Kane. (Sky Sports)
Hata hivyo, Bayern na Spurs bado wamesalia kuwa na tofauti kwenye thamani ya Kane kufuatia mazungumzo mapya, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 akitarajia kusalia katika klabu hiyo ya Ligi ya England. (Athletic)
Iwapo Kane ataondoka Tottenham klabu hiyo itafuatilia kumnunua mshambuliaji Gent wa Nigeria Gift Orban, 21, pamoja na beki mwingine wa kati na kiungo. (Times)
Mahasimu wa London Kaskazini, Arsenal na Tottenham wako tayari kupambana kumuwania kiungo wa kati wa Aston Villa Mbrazil Douglas Luiz, 25. (Football Insider)
Arsenal wamefikia makubaliano na Brentford ya kumsajili kipa wa Hispania David Raya, 27, kwa dau linalokaribia pauni milioni 30. (Fabrizio Romano)
Klabu ya Saudi Arabia Al-Hilal inataka kumsajili mshambuliaji wa Paris St-Germain na Brazil Neymar na inapanga kukutana na baba wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31. (Footmercato)
Neymar atakuwa tayari kuondoka PSG na kujiunga na klabu moja nchini Saudi Arabia ikiwa watamruhusu akae kwa mkopo Barcelona kwa msimu mmoja. (Sport)
Everton wanafikiria kumnunua mlinzi wa England Harry Maguire, 30, huku Manchester United ikimtaka kiungo wa kati wa Ubelgiji Amadou Onana, 21, kutoka upande wa pili. (Mirror)
Manchester United wanavutiwa na beki wa kati wa Ufaransa Jean-Clair Todibo kutoka Nice, 23, kama mbadala wa Maguire. (RMCSport)
Manchester United pia inataka kuanza mazungumzo rasmi ya mkataba mpya na beki Mwingereza Aaron Wan-Bissaka, 25, baada ya dirisha la usajili la sasa kufungwa. (Mail)
Beki wa kulia wa England Kyle Walker, 33, ameamua kusalia Manchester City, licha ya kufikia makubaliano ya awali ya kujiunga na Bayern Munich. (Athletic)
Real Sociedad wanataka kumchukua beki wa kushoto wa Arsenal na Scotland Kieran Tierney, 26, kwa mkopo msimu huu. (Telegraph) Barcelona wameongeza kipengele cha kutolewa cha euro 1bn (£861m)
kwenye mkataba wa kiungo wa kati wa Ujerumani Noah Darvich, 16. (Football transfers)
Kiungo wa kati wa Chelsea na Italia chini ya umri wa miaka 21 Cesare Casadei, 20, anasakwa kwa mkopo na Leicester City na Genoa. (Sky Sport via Football Italia)
Mshambulizi wa Uholanzi Wout Weghorst, 31, atajiunga na Wolfsburg kwa mkopo wa msimu mzima kutoka Burnley. (Bild)
BBC



