Michuano ya Ngao ya Jamii inaanza leo jijini Tanga ambapo mchezo wa kwanza wa nusu fainali ni kati ya mabingwa watetezi Yanga dhidi ya Azam Fc
Mchezo huo utapigwa saa 1 usiku katika uwanja wa Mkwakwani
Kwa mara ya kwanza mwaka huu, Ngao ya Jamii inashirikisha timu badala ya timu mbili kama ilivyokuwa imezoeleka huko nyuma
Mchezo wa pili wa nusu fainali kati ya Simba dhidi ya Singida FG unatarajiwa kupigwa kesho Alhamisi katika uwanja wa Mkwakwani
Mshindi wa mchezo wa leo atakutana na mshindi wa mchezo kesho kwenye fainali wakati timu zitakazopoteza zitachuana kusaka mshindi wa tatu
Michezo ya fainali na mshindi wa tatu itapigwa Jumapili, August 13



