Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kuwa klabu za Yanga, Simba na Singida FG hazitaruhusiwa kutumia wachezaji wa kigeni katika mechi za Ngao ya Jamii zinazoanza kupigwa jijini Tanga leo
Taarifa iliyotolewa na TFF mapema leo, imebainisha kuwa ni Azam Fc pekee ambayo imewasilisha vibali vya wachezaji 10 wa kigeni
