Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Alhamisi August 10 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
10 Aug 2023
Tetesi za soka Ulaya, Alhamisi August 10 2023

Manchester United wanatumai kumuunganisha tena Benjamin Pavard, 27, na mchezaji mwenza wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa, beki wa kati wa Mashetani Wekundu Raphael Varane, 30, kwa kutoa ofa ya euro 30m (£25.8m) kwa mlinzi huyo wa Bayern Munich. (L'Equipe)

Manchester United pia wana nia ya kumleta Sofyan Amrabat wa Fiorentina, huku raia huyo wa Morocco mwenye umri wa miaka 26 akipatikana kwa £30m. (Mail)

Hata hivyo, Amrabat anataka kujiunga na Atletico Madrid ya Diego Simeone msimu huu wa joto. (Sport)

Maafisa wa Paris St-Germain na mshambuliaji wa Brazil Neymar watakutana wiki hii katika jaribio la kutatua mustakabali wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31, na kusitishwa kwa mkataba wake ni miongoni mwa masuala yatakayojadiliwa. (UOL Sport Brasil)

Chelsea wanakaribia kumsajili kiungo wa Ecuador Moises Caicedo, 21, kutoka Brighton na wana nia ya kukamilisha usajili kwa wakati ili acheze mchezo wa ufunguzi wa ligi dhidi ya Liverpool siku ya Jumapili. (Guardian)

Kipa wa Chelsea Mhispania Kepa Arrizabalaga, 28, anasakwa na meneja wa zamani wa The Blues Thomas Tuchel aliyeko Bayern Munich huku timu hiyo ya Bundesliga ikitafuta mbadala wa Mjerumani Manuel Neuer mwenye umri wa miaka 37 ambaye ameumia. (Fabrizio Romano)

Chelsea wameamua kuachana na mazungumzo na Juventus kuhusu mkataba wa kubadilishana unaomhusisha mshambuliaji wa Serbia Dusan Vlahovic, 23, na mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 30. (Sky Sport Italia Via Football Italia)

Kipa wa Brentford na Hispania David Raya, 27, anatazamiwa kujiunga na Arsenal kwa mkopo akiwa na chaguo la kujiunga moja kwa moja msimu ujao, badala ya uhamisho wa kudumu. (Agthletic)

Arsenal wamekataa dau la pauni milioni 30 kutoka kwa Monaco inayoshiriki Ligue 1 kwa ajili ya mshambuliaji wao Mmarekani Folarin Balogun, 22. (90MIN)

Badala yake, Arsenal wanafikiria kuwatoa Balogun na mlinzi wa pembeni Mjapan Takehiro Tomiyasu, 24, kwenda Inter Milan ili kubadilishana na kiungo wao wa kati wa Italia Nicolo Barella, 26. (Calciomercato)

West Ham inashindana na Burnley kwa ajili ya kumnasa kwa mkopo mlinzi wa kushoto wa Chelsea Ian Maatsen, 21, ambaye alicheza kwa mkopo msimu uliopita akiwa na kikosi cha Vincent Kompany waliposhinda taji la Ubingwa. (Mail)

Burnley pia wanataka kumsajili beki wa pembeni wa Manchester United Mhispania Alvaro Fernandez kwa mkopo baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 kuonyesha kiwango kizuri akiwa Preston msimu uliopita. (Sky Sports via Twitter)

Wolves wanatarajiwa kukamilisha usajili wa beki wa West Ham Muingereza Aaron Cresswell, 33, kabla ya dirisha la usajili kufungwa. (Football Insider)

Mshambulizi wa Brighton raia wa Paraguay mwenye umri wa miaka 19, Julio Enciso anasakwa na mabingwa wa Italia Napoli. (Telegraph)

Bournemouth wako tayari kuingilia kati uhamisho wa Leeds United kwa beki wa kulia wa Norwich City Muingereza Max Aarons, 23. (Athletic)

Winga wa Leeds Wilfried Gnonto aliomba kuachwa nje ya kikosi chao kilichomenyana na Shrewsbury Town katika Kombe la Carabao Jumatano usiku huku Muitaliano huyo, 19, akitarajia kuhama. (Mail)

BBC

More Stories

Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
1h ago
READ MORE β†’
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
11h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
11h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
12h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
15h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
19h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
19h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
20h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
21h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
21h ago
READ MORE β†’