Chelsea wako tayari kuongeza ofa yao kwa kiungo wa kati wa Brighton Moises Caicedo baada ya Liverpool kuwasilisha dau la pauni milioni 111 kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ecuador mwenye umri wa miaka 21. (Guardian)
Dau hilo ambalo Chelsea wanajiandaa nalo linaweza kuwa na thamani pauni milioni £115 kutoka Uingereza. (Sky)
Liverpool ilimsajili Caicedo baada ya kupata hamasa kutoka kwenye kambi ya mchezaji huyo kwamba yuko tayari kwa uhamisho huo, lakini msimamo wa mchezaji huyo ulibadilika. (Mirror)
Chelsea inakaribia kukubaliana na mkataba wa kiungo wa kati wa Southampton mwenye umri wa miaka 19 Romeo Lavia wakati wakijaribu kumsajili Mbelgiji huyo na Caicedo. (Star)
Liverpool bado wanamtaka Lavia na wanatarajiwa kufanya mazungumzo zaidi na Southampton kuhusu mchezaji huyo. (Sky)
Hatua ya Chelsea kumleta kiungo wa kati wa Marekani mwenye umri wa miaka 24 Tyler Adams kutoka Leeds United kwa dau la pauni milioni 20 imekwama. (Sky)
Manchester City wanajiandaa kuwasilisha ombi jingine la kumsajili kiungo wa kati wa West Ham Lucas Paqueta baada ya kuwa na ofa ya awali ya pauni milioni 70 kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil mwenye umri wa miaka 25 kukataliwa. (Football)
The Hammers wanataka zaidi ya pauni milioni 90 kwa ajili ya Mbrazili huyo. (Telegraph)
Mlinzi wa Manchester City Joao Cancelo amerejea katika orodha ya wachezaji wanaosakwa na Barcelona, huku ajenti wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno mwenye umri wa miaka 29 akijaribu kupanga mpango huo. (Sport)
Aston Villa wanasubiri jibu kutoka kwa Galatasaray baada ya kufanya dau, ambalo linajumuisha ada ya mkopo ya euro milioni 3 na chaguo la euro milioni 20 kununua, kwa kiungo wa kati wa Italia Nicolo Zaniolo, 24. (Fabrizio Romano)
Arsenal imeweka bei ya pauni milioni 30 kwa mlinzi wa Japan mwenye umri wa miaka 24 Takehiro Tomiyasu, ambaye anamendewa na Inter Milan.
Sunderland wanataka mshambuliaji wa nyumbani mwenye umri wa miaka 16 Chris Rigg abaki kuwa "roho huru" huku Manchester United wakiwa na nia ya kumchukua. (Mirror)
Sheffield United imekubali mkataba wa pauni milioni 15 kumsajili kiungo wa kati wa Coventry City raia wa Brazil mwenye umri wa miaka 26 Gustavo Hamer. (Telegraph)
BBC