Mechi ya kwanza ya hatua ya awali kombe la Shirikisho barani Afrika kati ya Singida Fountain Gate FC dhidi ya Jku kutoka Zanzibar itachezwa Agosti 18,2023 kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi
Uongozi wa Singida FG, umetangaza mchezo huo hautakuwa na kiingilio, mashabiki wataingia bure
Afisa Habari wa Singida FG Hussein Masanza amesema kwa mashabiki wa timu hiyo kutoka Singida, watawapa usafiri wa kuwapeleka jijini Dar es salaam na kuwarudisha baada ya mchezo
