Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Alhamisi August 17 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
17 Aug 2023
Tetesi za soka Ulaya, Alhamisi August 17 2023

Liverpool wanaongeza juhudi zao za kumsajili kiungo wa kati wa Crystal Palace na Mali Cheick Doucoure, 23. (Independent) Liverpool pia wanatarajiwa kulipa euro 19m (£16.2m) kwa kiungo wa Stuttgart na Japan Wataru Endo, 30. (Athletic - subscription required)

Klabu hiyo pia imefufua nia yao ya kumnunua kiungo wa kati wa Uholanzi na Bayern Munich Ryan Gravenberch, 21. (Mail)

West Ham wanatathmini uwezekano wa kumsajili kiungo wa zamani wa Uingereza Jesse Lingard, 30, ambaye ni mchezaji huru baada ya kuachiliwa na Nottingham Forest baada ya mkataba wake kuisha. (Sky Sports, via Football Daily)

Kiungo wa kati wa Ureno Bernardo Silva, 29, ataongeza mkataba wake Manchester City kwa kitita cha euro 50m (£42.8m) msimu wa joto wa 2024. (El Chiringuito TV - in Spanish)

Chelsea imemuweka kiungo wa kati wa England chini ya umri wa miaka 21 Lewis Hall, 18, kuuzwa lakini inaomba kitita cha pauni milioni 30 huku Newcastle United ikionyesha nia. (Telegraph – Subscription Required)

Klabu ya Saudi Arabia Al-Hilal inakaribia kufikia makubaliano ya kumsajili Aleksandar Mitrovic, 28, kutoka Fulham baada ya kurejesha hamu yao ya kumnunua mshambuliaji huyo wa Serbia. (Guardian)

West Ham wanavutiwa na mshambuliaji wa Montpellier Mfaransa Elye Wahi, 20, Stuttgart na beki wa kati wa Ugiriki Konstantinos Mavropanos, 25, na beki wa Bayer Leverkusen na Ivory Coast Odilon Kossounou. (Guardian)

Mshambulizi wa Uhispania Ansu Fati, 20, ameripotiwa kuchagua kuondoka Barcelona, huku Manchester United, Arsenal na Tottenham zikiwa miongoni mwa klabu za Premier League zinazomwania. (AS – In Spanish)

Beki wa Ivory Coast Eric Bailly na Manchester United wamefikia makubaliano ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 kuondoka katika klabu hiyo bure msimu huu wa joto, huku Fulham wakiripotiwa kumtaka. (RMC Sport, via French)

Kipa wa Uhispania na wakala huru David de Gea, 32, anatamani kuhamia Bayern Munich baada ya kuondoka Manchester United msimu huu. (Mirror)

Tottenham wanamfikiria Mhispania Mateu Alemany, ambaye ataondoka Barcelona mwezi Septemba, kama chaguo linalowezekana kwa mkurugenzi wao mpya wa soka. (Fabrizio Romano)

Nia ya Bournemouth ya kutaka kumsajili kiungo wa kati wa Marekani Tyler Adams, 24, kutoka Leeds United inaonekana kupungua. (Subscription Required)

Mshambulizi wa Brazil Neymar, 31, inasemekana aliomba jumba la vyumba 25, bwawa la kuogelea na sauna, wafanyakazi wanane kuweka nyumba yake katika hali ya usafi, magari tisa na gharama zote zilizolipwa kwa usafiri, mikahawa na hoteli wakati aliposaini klabu ya Saudi Pro League Al- Hilal. (Cope, via Goal)

BBC

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
39m ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
51m ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
1h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
4h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
8h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
8h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
9h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
10h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
10h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
11h ago
READ MORE β†’