Yanga - Asas - Local

Gamondi akiri kutowafahamu ASAS Fc

Joel JJ By Joel JJ
β€’
19 Aug 2023
Gamondi akiri kutowafahamu ASAS Fc

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema wamekamilisha maandalizi tayari kwa michuano ya ligi ya mabingwa hatua ya awali, kesho wakitarajia kuchuana na Asas Fc ya Djibout

Gamondi amesema pamoja na kuwa hawawafahamu vyema wapinzani wao, wamejiandaa kikamilifu tayari kwa kukabiliana nao kwani anaamini ni timu nzuri

"Tumekamilisha maandalizi ya mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa dhidi ya Asas Fc. Hatuwafahamu vyema wapinzani wetu lakini tumefanya maandalizi kikamilifu naamini tutakuwa na mchezo mzuri na matokeo mazuri pia"

Gamondi amesema baada ya michuano ya Ngao ya Jamii, wamepata muda wa kufanya maboresho maalum ya kiufundi hivyo mashabiki wa Yanga watarajie burudani na mchezo mzuri utakaoambatana na magoli

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake, mlinzi wa kushoto Nickson Kibabage amesema wanakwenda kwenye mchezo huo wakiwa na dhamira ya kushinda

"Sisi hatudharau timu yoyote, tunajua tunakutana na timu ambayo ni bingwa huko kwao hivyo tunauchukulia mchezo huu kwa uzito kama mechi nyingine yoyote," alisema

Mchezo huo wa mkondo wa kwanza hatua ya awali michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika, utapigwa Jumapili August 20 saa 11 jioni katika uwanja wa Azam Complex, Asas Fc wakiwa wenyeji wa mchezo huo

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
46m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’