Yanga yaanza vyema Ligi ya Mabingwa, Azam yapoteza ugenini

Joel JJ By Joel JJ β€’ 20th August 2023


Yanga yaanza vyema Ligi ya Mabingwa, Azam yapoteza ugenini

Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika, Yanga wameanza vyema michuano hiyo baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Asas Fc ya Djibout

Mabao ya Stephane Aziz Ki na Kennedy Musonda yameihakikishia Yanga kupata ushindi muhimu katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa uwanja wa Azam Complex

Yanga ina nafasi nzuri ya kusonga mbele raundi ya kwanza ikihitaji ushindi au matokeo yoyote ya sare katika mchezo wa marudiano utakaopigwa uwanja wa Azam Complex wiki ijayo

Wawakilishi wengine wa Tanzania katika kombe la Shirikisho Azam Fc wamepoteza ugenini kwa kukubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Fasil Dar Kenema ya Ethiopia

Azam Fc wanahitaji ushindi wa angalau bao 1-0 katika mchezo wa marudiano utakaopigwa August 25 uwanja wa Azam Complex


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.