Simba - Local

Robertinho atoa siku nne za mapumziko Simba

Joel JJ By Joel JJ
β€’
24 Aug 2023
Robertinho atoa siku nne za mapumziko Simba

Kufuatia Ligi Kuu kutarajiwa kusimama mwishoni mwa wiki kupisha kalenda ya mechi za Kimataifa, wachezaji wa Simba walipewa mapumziko kuanzia jana Jumatano na watarejea kambini Jumapili

Awali Simba iliendelea na ratiba wa maandalizi yake ikiwa na matarajio ya Bodi ya Ligi kuridhia ombi la mchezo dhidi ya Coastal Union kupigwa siku ya Ijumaa lakini mchezo huo utapangiwa tarehe mwezi ujao baada ya kalenda ya mechi za Kimataifa

Afisa Habari wa TPLB, Karim Boimanda amesema imekuwa ngumu kubadili ratiba kutokana na muingiliano wa mechi ya timu ya Taifa Stars inayotarajia kuchezwa kuanzia Septemba 4 hadi 12 mwaka huu ambapo Stars watacheza na Algeria

"Ni kweli waliandika barua ya kuomba mechi ichezwe Ijumaa lakini sababu ya mechi hiyo kutopangiwa tarehe ama kutochezwa hiyo Ijumaa waliyoomba Simba ni kutokana na ratiba ya Taifa Stars ambao wana mechi ya kufuzu"

"Kikawaida kocha wa timu ya taifa anatakiwa aingize timu kambini wiki kama mbili kabla ya mechi. Sasa wiki hizi zipo ndani ya ratiba ya Taifa Stars, kikanuni pia ni kwamba timu ikitoa wachezaji watatu kwenda timu ya taifa basi mechi zake zinasogezwa na Simba huenda wakatoa wachezaji hao"

"Hivyo hapa ratiba inatubeba wote ili tuwe salama, bodi na timu, maana kama tungeipangia tarehe hiyo mechi na ikatokea Simba imetoa wachezaji zaidi ya watatu wana uwezo wa kugomea mechi kuwa hawatacheza wachezaji wao wapo timu ya taifa,"

"Hivyo hadi muda huu ratiba ipo pale pale, Simba wasubiri hadi bodi itakapopanga tarehe ya mechi hiyo, ukiangalia pia Coastal wamewapa mapumziko wachezaji wao," Boimanda amenukuliwa na gazeti la Mwanaspoti

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
6h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
6h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
7h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
10h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
14h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
14h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
15h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
16h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
16h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
17h ago
READ MORE β†’