Simba mguu sawa kukabiliana na vigogo Afrika

Joel JJ By Joel JJ β€’ 28th August 2023


Simba mguu sawa kukabiliana na vigogo Afrika

Droo ya African Football League (Super League) inatarajiwa kufanyika Septemba 02 huko Misri

Simba ni miongoni mwa timu nane ambazo zitashiriki michuano hiyo maalum ambayo inafanyika kwa mara ya kwanza barani Afrika

Timu zimewekwa katika makundi mawili ya timu nne kulingana na alama walizokusanya katika mashindano ya CAF miaka mitano iliyopita

Kundi A lina timu za Al Ahly, Mamelod Sundowns, Wydad Athletic na Esperace

Kundi B lina timu za Simba, TP Mazembe, Enyimba na Perto Luanda

Timu za kundi moja hazitakutana kwenye hatua ya awali kwa maana timu kutoka kundi A itapangwa kuchuana na timu kutoka kundi B

Simba itafungua michuano hiyo Oktoba 20 kwa kuchuana na Al Ahly, Mamelod Sundowns, Wydad au Esperance


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.