Tetesi za soka Ulaya, Alhamisi August 31 2023

Joel JJ By Joel JJ β€’ 31st August 2023


Tetesi za soka Ulaya, Alhamisi August 31 2023

Al-Ittihad wanaandaa dau la pauni milioni 118 kwa ajili ya Mohamed Salah, licha ya Liverpool kusisitiza kwamba mshambuliaji huyo raia wa Misri mwenye umri wa miaka 31 hauzwi. (Mail)

Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp atakasirika ikiwa timu hiyo itashawishiwa kukubali ofa ya Al-Ittihad ya Saudia kwa ajili ya Salah wakati tarehe ya mwisho ya dirisha la uhamisho ni siku ya Ijumaa. (Star)

Tottenham Hotspur iko kwenye mazungumzo na Barcelona kuhusu mkataba wa mkopo kwa msimu mzima kwa mshambuliaji wa Uhispania Ansu Fati, 20. (Fabrizio Romano)

Brighton wamemtafuta Fati, huku Chelsea na Borussia Dortmund wakiwa miongoni mwa vilabu vingine vinavyomkodolea macho. (Mundo Deportivo)

Spurs pia wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Crystal Palace, Muingereza, Eberechi Eze, 25, baada ya uhamisho wa mshambuliaji wa Nottingham Forest, Brennan Johnson, 22, kukwama. (Independant)

Manchester United wanataka kusajili kiungo kabla ya tarehe ya mwisho, huku mchezaji wa kimataifa wa Morocco wa Fiorentina, Sofyan Amrabat, 27, akiwa lengo lao kuu. (Mirror)

Fiorentina wamekataa ofa ya mkopo ya United ya pauni milioni 1.7 kwa Amrabat lakini wanaweza kumuuza ikiwa watakuwa na lengo la kumnunua moja kwa moja. (Mail)

Manchester United pia wamewasiliana na Tottenham kuhusu kumnunua kiungo wa kati wa Denmark, Pierre-Emile Hojbjerg, 28. (Sky Sports)

Bayern Munich wamefanya mazungumzo na Chelsea katika jitihada za kumsajili beki wao Mwingereza, Trevoh Chalobah, 24. (Athletic) Luton Town iko tayari kumsajili beki wa Manchester United Muingereza, Teden Mengi, 21. (Mail)

Nottingham Forest inakaribia kufikia makubaliano ya kumchukua winga wa Uingereza, Callum Hudson-Odoi, 22, kutoka Chelsea. (Guardian)

Sheffield United wanaongoza katika mbio za kumsajili kiungo wa kati wa Manchester City na England, James McAtee, 20, kwa kipindi cha pili cha mkopo katika klabu hiyo baada ya kukaa Bramall Lane msimu uliopita. (Football Insider)

Al-Ittihad wamempigia simu beki wa Liverpool, Mfaransa, Ibrahima Konate 24, kuhusu uwezekano wa kuhama. (RMC Sport)

Bayern Munich wanatazamiwa kuzindua ombi la kutaka kumsajili mchezaji wa kimataifa wa Ureno mwenye umri wa miaka 28, Joao Palhinha. (Standard)

Katika mkataba wa pauni milioni 35 ambao ulimchukua mshambuliaji wa Marekani, Folarin Balogun mwenye umri wa miaka 22 kwenda Monaco, Arsenal ilikubali 17.5% ya mauzo ikiwa mchezaji huyo atauzwa kwenda klabu ya tatu. (Mirror)

BBC


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.