Simba - Local

Ahmed Ally atamba, Al Ahly wameyakanyaga AFL

Joel JJ By Joel JJ
4 Sep 2023
Ahmed Ally atamba, Al Ahly wameyakanyaga AFL

Baada ya Simba kumfahamu mpinzani wake katika michuano ya African Football League, SImba imeanza mkakati wa kuhakikisha inafanya vizuri katika michuano hiyo 

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ally amesema Wanasimba walisubiri kwa hamu droo hiyo iliyofanyika juzi JUmamosi huko Misri na kila mmoja amefurahi baada ya kupangwa kuikabili Al Ahly, mabingwa wa Afrika

Ahmed amesema furaha ya Wanasimba inatokana na historia yao ya kuwanyanyasa Al Ahly nyakati zote walipokuja Tanzania kucheza dhidi ya Simba

"Tulisubiri kwa hamu droo hii na sasa tumemfahamu mpinzani wetu ni Al Ahly, tumefurahi sana. Tunawakaribisha Dar, sisi tunataka kusimika ububwa wetu katika soka la Afrika, sasa ili uwe mkubwa lazima uwafunge wakubwa wenzio"

"Uzuri hata wao wanafahamu uchungu wa kucheza na Simba uwanja wa Benjamin Mkapa, wamepasuka mara mbili kwa mabao ya Meddie Kagere na Jose Luis Miquissone kilichobadlika ni kuondoka kwa Kagere lakini makali ya Simba yako palepale"

"Tunafahamu, ukitaka kuwa mkubwa jela lazima umpige bwana jela, kwa hiyo tunamkaribisha Al Ahly na tunamuhakikishia kwamba tutahangaika nae"

"Super Ligi hairuhusiwi kwa watoto wadogo, hii ni kwa ajili ya wakubwa pekee na Simba Sc ni mkubwa, kwa hiyo hatuna mashaka, hatuna hofu, hatuna wasiwasi wala hatuna woga, " alitamba Ahmed

More Stories

Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa uhuru
52m ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
55m ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
1h ago
READ MORE →
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
1h ago
READ MORE →
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
1h ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
3h ago
READ MORE →
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
13h ago
READ MORE →
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
13h ago
READ MORE →
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
14h ago
READ MORE →
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
17h ago
READ MORE →