Ngome Fc yakana kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Simba

Joel JJ By Joel JJ β€’ 9th September 2023


Ngome Fc yakana kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Simba

Klabu ya Ngome Fc kutoka visiwani Zanzibar imekana kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Simba leo

Mapema leo Simba ilitangaza kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Ngome Fc na kuibuka na ushindi wa mabao 6-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Mo Simba Arena

Taarifa iliyotolewa na timu hiyo kupitia kurasa za mitandao ya kijamii, iliitaka klabu ya Simba kuthibitisha kama walicheza mechi hiyo au kurekebisha taarifa waliyotoa mapema siku ya Jumamosi

Hata hivyo klabu ya Simba ilisahihisha na kubainisha kuwa ilicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Ngome Fc ya jijini Dar es salaam

Simba iliibuka na ushindi wa mabao 6-0 katika mchezo huo, mabao yakifungwa na Jean Baleke aliyefunga mawili, Shomari Kapombe, Aubin Kramo,, Willy Onana na Shabani Idd Chilunda

Huo ulikuwa mchezo wa mwisho wa kirafiki kwa Simba kabla ya kuelekea Zambia wanakokabiliwa na mchezo wa ligi ya mabingwa kuwania tiketi ya kutinga hatua ya makundi dhidi ya Power Dynamos utakaopigwa Septemba 16 huko Zambia


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.