Bodi ya Ligi Kuu imeipangia tarehe michezo ambayo ilisogezwa mbele kupisha kalenda ya mashindano ya CAF na FIFA
Kulingana na taarifa iliyotolewa na TFF mapema leo, mchezo kati ya Yanga dhidi ya Namungo Fc utapigwa Septemba 20 katika uwanja wa Azam COmplex
Mchezo kati ya Simba dhidi ya Coastal Union utapigwa Septemba 21 katika uwanja wa Uhuru wakati pia mchezo kati ya Azam Fc dhidi ya Singida FG nao ukipigwa katika uwanja wa Azam Complex
Hata hivyo tarehe hizo zinaweza kubadilika kama CAF itathibitisha uwepo wa mechi za mashindano ya CHAN yanayohusisha wachezaji wa ndani
Kulingana na kalenda ya CAF, mechi hizo zinapaswa kuanza mwishoni mwa mwezi Septemba 2023




