Singida - Local - Transfer

Tambwe aitega Singida FG

Joel JJ By Joel JJ
β€’
17 Sep 2023
Tambwe aitega Singida FG

Mshambuliaji Amissi Tambw ameuandikia barua uongozi wa Singida FG akiupa siku saba ili ukamalishe madai yake kabla hajatimkia Shirikisho la Kimataifa la Soka (FIFA) kushtaki

Tambwe alitemwa na Singida FG katika dirisha la usajili lililopita lakini mwenyewe amesema bado ana mkataba wa mwaka mmoja na klabu hiyo

"Bado nina mkataba wa mwaka mmoja na Singida, ila wamenisitishia bila ya mazungumzo na cha kushangaza nalipwa mshahara wangu kila mwezi, lakini madai yangu ya fedha za usajili hayafanyiwi kazi"

"Nimeongea na Mwanasheria wangu ameniambia tayari amewatumia barua kuwaamuru wanilipe fedha yangu ndani ya siku saba tangu aitume barua hiyo na kama watashindwa kufanya hivyo mpango wangu ni kwenda FIFA,"alisema Tambwe

Tambwe amefunguka kuwa baada ya msimu uliopita kumalizika alirudi kwao Burundi kwa mapumziko na muda wa kurudi ulipowadia ili kujiandaa na msimu mpya alizungumza na uongozi juu ya kutumiwa tiketi ya ndege lakini walikuwa wakimuahidi bila utekelezaji, kabla ya kuambiwa hatakuwa tena na timu hiyo

"Sikutumiwa tiketi, ila baadaye tulifanya mazungumzo na nikaambiwa hawatakuwa nami kikosini kwa msimu huu bila sababu yoyote na kukubaliana kunipa madai yangu, lakini hadi sasa hawajafanya hivyo na wamekuwa wakiniingizia mshahara kama kawaida"

"Shida yangu ni kulipwa fedha yangu ya usajili ya msimu mmoja uliobaki ambao naingiziwa mshahara kama makubaliano yetu yalivyokwenda shida ni fedha ya usajili ambayo taarifa yake ipo kwa mwanasheria wangu na ameifanyia kazi kwa kuutaka uongozi kunilipa kama makubaliano yetu yalivyokuwa"

More Stories

Mizzima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizzima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
10m ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
3h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
4h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
4h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
5h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
6h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
7h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
7h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
20h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
20h ago
READ MORE β†’