Yanga - Local

Yanga kuwaenzi waliosafiri Rwanda

Joel JJ By Joel JJ
β€’
18 Sep 2023
Yanga kuwaenzi waliosafiri Rwanda

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amewataka Wanachama na Mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo Fc ambao utapigwa Jumatano, Septemba 20 katika uwanja wa Azam Complex

Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari mapema leo, Kamwe alitangaza kuwa mchezo huo watautumia kuwaenzi mashabiki waliosafiri kwa wingi kwenda Rwanda kuishangilia Yanga kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Merrikh ambao Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-0

Kamwe alitangaza viingilio vya mchezo huo ambapo VIP A ni Tsh 20,000/-, VIP B ni Tsh 10,000/- na Mzunguuko ni Tsh 5,000/-

"Yanga imekuwa klabu ya kwanza barani Afrika kusafiri na mashabiki wengi katika mechi ya ugenini na kujaza uwanja. Hili ni jambo lililotupa heshima kubwa Afrika nzima na hivyo tumeufanya mchezo dhidi ya Namungo Fc kuwa maalum kwa ajili ya mashabiki waliosafiri Rwanda"

"Tumeandaa utaratibu siku ya Jumatano ambapo itakapofika dakika ya 12 mashabiki wote watasimama na kupiga makofi kwa dakika moja ikiwa ni ishara ya kuwapongeza wote waliosafiri na timu Rwanda"

"Uongozi pia umeandaa surprise kwenye dakika ya 12 ambayo itaonekana uwanjani na Azam Tv kwa wale ambao hawatakuwa uwanjani. Tunawaomba hata wale ambao watakuwa nyumbani au katika vibanda umiza wasimame kwenye dakika ya 12 kuwapa maua yao wale waliosafiri Rwanda," alisema Kamwe

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
5h ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
8h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
10h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
12h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
14h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
15h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
15h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
17h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
20h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
1d ago
READ MORE β†’