Mtanzania mwingine aweka rekodi UEFA CL

Joel JJ By Joel JJ β€’ 20th September 2023


Mtanzania mwingine aweka rekodi UEFA CL

Mlinzi kiraka wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Novutus Dismus jana alicheza kwa dakika 90 mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya uliokutanisha timu yake Shakhtar Donestk dhidi ya Porto

Novutus alitumika kama mlinzi wa kushoto na baadae kuhamishiwa safu ya ulinzi wa kati timu yake ikikubali kipigo cha mabao 3-1 nyumbani

Nova anakuwa mchezaji wa tatu mTanzania kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya baada ya Kassim Manara na Mbwana Samatta

Shakhtar imepangwa kundi H katika michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya ikiwa sambamba na Porto, Antwerp na Fc Barcelona

Mchezo wao utakaofuata kwenye michuano hiyo ni Oktoba 04 ugenini dhidi ya Antwerp


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.