Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Jumatano Septemba 27 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
27 Sep 2023
Tetesi za soka Ulaya, Jumatano Septemba 27 2023

Mkurugenzi wa michezo wa Arsenal Edu amefanya mazungumzo na wakala wa mshambuliaji wa Aston Villa Ollie Watkins kuhusu uhamisho wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza, 27, huku Chelsea pia ikimtaka mchezaji huyo. (Football Transfers)

Aston Villa wamesalia kwenye mazungumzo kuhusu kuongeza mkataba wa Watkins na wanataka mkataba mpya ukamilishwe ifikapo Januari. (90 min)

Arsenal na Chelsea wako tayari kutoa wachezaji pamoja na pesa katika majaribio yao ya kumsajili mshambuliaji wa Uingereza Ivan Toney kutoka Brentford, ambaye kuna uwezekano wa kutaka zaidi ya £75m kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27. (90 min)

Newcastle United wanatazamiwa kuanza mazungumzo na kiungo wa kati wa Brazil Joelinton, 27, na kiungo wa kati wa Uingereza Sean Longstaff, 25, kuhusu kuongeza kandarasi zao, ambazo zote zinatazamiwa kumalizika Juni 2025. (Football Insider)

Barcelona wanafikiria kumnunua kiungo wa kati wa Nigeria Wilfred Ndidi, 26, wakati kandarasi yake Leicester City itakapokamilika mwishoni mwa msimu huu. (Sport - kwa Kihispania)

Napoli wanamfuatilia meneja wa zamani wa Paris St-Germain Christophe Galtier kufuatia mwanzo mbaya wa msimu chini ya Rudi Garcia, wakati Marseille pia wanavutiwa na mchezaji huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 57 baada ya kocha wa zamani Marcelino kujiuzulu kwa kushtukiza. (RMC Sport – In French)

Bilionea wa Uingereza Sir Jim Ratcliffe yuko tayari kurekebisha ofa yake ya kuinunua Manchester United ili kufikia makubaliano na wamiliki wa sasa wa Glazers. (Mirror)

Barcelona wamekubali kwa mdomo wa ada ya euro 35m (£30.4m) na Manchester City kubadilisha mkopo wa beki wa pembeni wa Ureno Joao Cancelo kuwa mkataba wa kudumu. (El Chiringuito TV - Spanish)

Mshambulizi wa Slovenia Benjamin Sesko, 20, anasema alizungumza na Manchester United msimu uliopita kabla ya kuondoka Red Bull Salzburg, lakini alihisi kuhamia RB Leipzig kulikuwa bora ili kujiimarisha. (Transfermarkt - Germany)

Reading wamewekewa vikwazo vya kuhama kwa kushindwa kulipa HMRC kwa wakati na wanaweza kukabiliwa na kukatwa pointi zaidi ikiwa watashindwa kulipa mishahara kwa wachezaji na wafanyakazi Ijumaa hii. (Telegraph – Subscription Required)

Chelsea imepewa kibali cha Ligi Kuu ya Uingereza kwa kampuni ya data za michezo ya Infinite Athlete kuwa mdhamini wao wa mbele ya jezi katika mkataba wa thamani ya takriban £40m kwa msimu huu. (Telegraph – Subscription Required)

BBC

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
10h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
10h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
10h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
14h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
17h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
18h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
18h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
19h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
20h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
21h ago
READ MORE β†’