Simba - Local

Power Dynamos kutua leo, Simba iko tayari

Joel JJ By Joel JJ
β€’
28 Sep 2023
Power Dynamos kutua leo, Simba iko tayari

Kikosi cha Simba kinaendelea kujifua Mo Simba Arena tayari kwa mchezo muhimu wa kuwania tiketi ya kutinga hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Power Dynamos

Mchezo huo utaunguruma siku ya Jumapili, Oktoba 1 katika uwanja wa Azam Complex majira ya saa 10 jioni

Wapinzani wao Power Dynamos tayari wameondoka Zambia kuja nchini ambapo timu hiyo ilitarajiwa kuwasili saa 12

Vijana wa Kocha Robertinho Oliveira wanajiandaa kushinda mchezo huo wakifahamu matokeo hayo yatatosha kuwapeleka makundi

Sare ya mabao 2-2 katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Zambia, yameiweka Simba katika nafasi nzuri ya kufuzu kwani hata matokeo ya 0-0 au 1-1 yatatosha kuwavusha wekundu hao wa Msimbazi

Mkufunzi wa Simba Robertinho amesema maandalizi kuelekea mchezo huo yanaendelea vizuri, anaridhishwa na ari, morali ya wachezaji wake

"Tunafanya maandalizi muhimu, lengo letu ni kucheza vizuri na kupata ushindi mnono. Tutacheza nyumbani mbele ya mashabiki wetu, hii ni mechi muhimu sana kwetu"

"Nafurahi wachezaji wako tayari, ari na morali yao mazoezini ni kubwa, wanafahamu kwa ukubwa wa klabu ya Simba, wanapaswa kushinda na kukata tiketi ya kutinga makundi"

"Najua mchezo hautakuwa mwepesi kwa sababu Power Dynamos ni timu nzuri lakini niwaambie, Simba ni timu kubwa barani Afrika na tutaonyesha ukubwa wetu," alisema Robertinho

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
38m ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
50m ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
1h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
4h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
8h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
8h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
9h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
10h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
10h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
11h ago
READ MORE β†’