Tanzania iko kwenye nafasi nzuri ya kuwa na timu mbili kwenye hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabinwa Afrika baada ya Yanga kukata tiketi jana kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Al Merrikh
Leo watani zao Simba nao watashuka uwanja wa Azam Complex katika mchezo muhimu ambao ushindi utaihakikishia Simba kwenda makundi
Sare ya mabao 2-2 waliyopata kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Zambia, unaipa Simba nafasi nzuri zaidi ya kutinga makundi ikihitaji ushindi au hata matokeo ya sare isiyozidi bao moja
Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari jana, Mkufunzi wa Simba Robertinho Oliveira alisema wamepata muda mzuri wa kufanya maandalizi hivyo ana matumaini makubwa ya ushindi leo
Pamoja na kumkosa beki kisiki Hennock Inonga Baka, Robertinho alisema tayari amemuandaa mchezaji wa kuchukua nafasi yake hivyo hakuna wasiwasi
Matumaini ya Wanasimba ni ushindi siku ya leo na kukata tiketi ya kutinga hatua ya makundi