Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Jumatatu Oktoba 02 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
2 Oct 2023
Tetesi za soka Ulaya, Jumatatu Oktoba 02 2023

Matumizi makubwa ya Chelsea yanatazamiwa kuendelea Januari huku klabu hiyo ikimlenga mshambuliaji wa Napoli mwenye umri wa miaka 24 Victor Osimhen na mshambuliaji wa Brentford wa Uingereza Ivan Toney, 27. (Guardian)

Chelsea pia wanatafuta mkopo wa pauni milioni 500 ili kufadhili usajili huo baada ya kutumia pauni bilioni 1 katika kipindi cha madirisha matatu ya uhamisho.(Sun)

Arsenal itamgeukia kiungo wa kati wa Manchester City na Uingereza Kalvin Phillips mwenye umri wa miaka 27 mwezi Januari huku The Gunners wakipania kuimarisha safu yao ya kati. (Fichajes - Kwa Kihispania)

Winga wa Barcelona mwenye umri wa miaka 16 kutoka Uhispania Lamine Yamal anatazamiwa kusaini mkataba mpya wa miaka mitatu na klabu hiyo, ambao una kipengele cha kuachiliwa kwa pauni 1bn (Fabrizio Romano)

Newcastle wanamfuatilia mlinzi wa Crystal Palace wa Denmark Joachim Andersen kwa nia ya kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 mwezi Januari. (Football Insider)

Barcelona wako tayari kumuuza mshambuliaji wa Uhispania Ansu Fati msimu ujao wa joto baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 kumaliza muda wake wa mkopo Brighton (Sport - in Spanish)

Lionel Messi ameitaka Inter Miami kumsajili kiungo wa kati wa Real Madrid na Croatia Luka Modric, 38. (Cadena Ser - Kwa Kihispania , kupitia Mirror)

Liverpool wamekubaliana kimsingi na beki wa Uingereza Trent Alexander-Arnold kwa mkataba mpya, ambao utamfanya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 kulipwa zaidi ya £200,000 kwa wiki, pamoja na bonasi. (Football Insider)

Barcelona wameanza mazungumzo na Corinthians kwa ajili ya kumnunua kiungo wa kati wa Brazil mwenye umri wa miaka 18 Gabriel Moscardo huku wakitarajia kuipiku Chelsea kwenye usajili wake(Sport via Goal)

Juventus wanatumai kumfunga kiungo wa kati wa Ufaransa Adrien Rabiot, 28, kwa kandarasi mpya ya miaka mitatu baada ya kukataa ripoti kwamba anataka kuhamia Manchester United msimu wa joto ili kusaini mkataba wa mwaka mmoja zaidi(Tuttosport)

Tottenham itatafuta kumsajili beki wa Bayern Leverkusen mwenye umri wa miaka 24 wa Burkina Faso Edmond Tapsoba mwezi Januari (Fichajes - Kwa Kihispania)

Kiungo wa kati wa vijana wa Uingereza Dan Rigge, 17, anatazamiwa kusaini mkataba mpya wa muda mrefu katika klabu ya West Ham , licha ya vilabu vinne vya Ligi ya Premia na mbili za La Liga kutaka huduma zake (Fabrizio Romano)

BBC

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
39m ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
51m ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
1h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
4h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
8h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
8h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
9h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
10h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
10h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
11h ago
READ MORE β†’