Liverpool wana nia ya kumsajili winga wa Wolves na Ureno Pedro Neto, 23, ikiwa mshambuliaji wa Misri Mohamed Salah, 31, ataondoka msimu ujao. (Foobal Transfers)
Arsenal, Aston Villa na Atletico Madrid pia wanataka kumsajili Neto. (90mins)
Mkufunzi wa Manchester United Erik ten Hag ameweka nia ya kutaka kusajili wachezaji kadhaa Januari mwakani. (Football Insider)
Mmoja wao ni beki wa Sporting Lisbon na Ureno Goncalo Inacio, huku United wakituma wasaka vipaji wao kumfuatilia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22. (Sun)
Mkurugenzi wa michezo wa Bayer Leverkusen Simon Rolfes anasema kocha Xabi Alonso, 41, "anaangazia" klabu hiyo ya Ujerumani baada ya kiungo huyo wa zamani wa Liverpool kuhusishwa na tetesi za kuchukua mikoba ya Carlo Ancelotti katika klabu ya Real Madrid. (Mail)
Barcelona wanapania kumjumuisha mshambuliaji wa Athletico Paranaense na Brazil Vitor Roque, 18, katika klabu hiyo mwezi Januari badala ya Julai huku mkurugenzi wa michezo Deco akipanga kusafiri hadi Brazil wakati wa mapumziko yajayo ya kimataifa. (Goal)
Wasiwasi mpya umeibuliwa juu ya wamiliki wapya watarajiwa wa Everton 777 Partners, baada ya klabu ya Vasco da Gama ya Brazil, klabu yake nyingine, kushindwa kulipa malipo ya uhamisho wa wachezaji watatu uliogharimu jumla ya pauni milioni 4.5. (Guardian)
Liverpool wanamtaka beki wa kati wa Brazil wa chini ya miaka-20 Lucas Beraldo, 19, na wametuma maskauti kumfuatilia akiichezea Sao Paulo mara kadhaa. (90mins)
West Ham wanajadiliana na winga wa Uingereza Jarrod Bowen, 26, kuhusu mkataba mpya huku Liverpool ikionyesha nia ya kutaka kumsajili. (Football Insider)
Arsenal wameanza kujadiliana na beki wa Uingereza Ben White kuhusu mkataba mpya, licha ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kusalia na miaka mitatu kwenye mkataba wake wa pauni 120,000 kwa wiki. (Mail)
Mshambulizi wa Ubelgiji Lois Openda, 23, ambaye Arsenal alimnyatia katika dirisha la usajili la majira ya joto, ana kipengele cha kutolewa katika kandarasi yake ya RB Leipzig ya takriban pauni milioni 70 ambayo inaweza kuanzishwa mwaka wa 2025. (Sky Germany via X)
Klabu ya Saudi Pro League Al Nassr ina mpango wa kumsaka kiungo wa Roma Bryan Cristante mwenye umri wa miaka 28 katika dirisha la uhamisho wa Januari. (Calcio Mercato - kwa Kiitaliano)
BBC



