Spurs, Arsenal zaweka rekodi Premia Ligi

Joel JJ By Joel JJ β€’ 9th October 2023


Spurs, Arsenal zaweka rekodi Premia Ligi

Klabu ya Arsenal na Tottenham Hotspur zote zikiwa zinatokea London ndio timu pekee kwenye ligi kuu ya England hazijapoteza mchezo wowote mpaka sasa kwenye michezo 8 waliyocheza

Arsenal imedroo michezo miwili mmoja dhidi ya Fulham na mwingine dhidi ya Tottenham Hotspur huku Tottenham Hotspur ikidroo michezo miwili pia mmoja dhidi ya Brentford na mwingine ni dhidi ya Arsenal kwenye London derby

Ligi ya Uingereza imesimama kupisha ratiba ya timu za taifa na itarejea baada ya wiki mbili

Jana Arsenal ilifuta uteja dhidi ya Manchester City kwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Emirates

Licha ya ushindi huo Arsenal wamebaki nafasi ya pili nyuma ya Spurs inayoongoza ligi baada ya kukusanya alama 20 na faida ya mabao 18 ya kufunga na kufungwa mabao nane

Arsenal wana alama 20, wamefunga mabao 16 na kuruhusu mabao sita wakitofautiana kwa mabao tu na mahasimu wao kutoka jiji la London


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.