Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Mbwana Samatta amesema mchezo wa kirafiki dhidi ya Sudan uliopigwa Saudi Arabia jana ni kipimo kizuri kuelekea mashindano makubwa
Jana Stars ililazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Sudan katika mchezo uliopigwa huko Saudi Arabia. Mchezo huo uko kwenye kalenda ya FIFA
Samatta alisema kabla ya mchezo huo kocha aliwaambia kuna vitu alitaka kuviona katika mchezo huo ambavyo vitamsaidia katika maandalizi kuelekea mashindano makubwa
"Nafikiri ni kipimo kizuri kwetu wachezaji na benchi la ufundi. Kabla ya mchezo kocha alituambia kuna vitu alitaka kuviona katika mchezo huu na naamini ameviona"
"Naamini utatusaidia katika maandalizi kuelekea mashindano makubwa yanayokuja mbele yetu," alisema Samatta
Mwezi Novemba 2023 Stars inakabiliwa na mechi mbili za kuwania kufuzu michuano ya kombe la Dunia dhidi ya Niger na Morocco kabla ya kuelekea Ivory Coast kwenye michuano ya Afcon 2023 mwezi Januari 2024