Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ally leo ameongoza hamasa za mtaa kwa mtaa kuelekea mchezo wa AFL dhidi ya Al Ahly ambao utapigwa Ijumaa, Oktoba 20 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Ahmed leo alikuwa na kazi mbili, mosi ni kuwahamasisha mashabiki kununua tiketi ili kuhakikisha wanaujaza uwanja wa Benjamin Mkapa
Lakini pia Ahmed aliendesha zoezi la kulipamba jiji la Dar es salaam ambapo stika za mchezo kati ya Simba dhidi ya Al Ahly zilibandikwa katika maeneo yota ambayo hamasa ilikuwa ikifanyika
Msafara ulifika Mbezi, kituo cha Mabasi Magufuli na kupokelewa na umati wa mashabiki wa Simba ambao wamehamasika kuelekea mchezo huo
Ahmed ametamba siku ya Ijumaa ni maalum kwenda kuwavutisha pumzi ya moto Al Ahly ambao wanatarajiwa kuwasili nchini kesho Jumanne
"Tumeshakuwa wababe kwenye mechi hizi kubwa. Muhimu ni mashabiki wote kujitokeza kwa wingi tarehe 20 twendeni tukamuwashie Al Ahly moto," alisema Ahmed








