Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Jumanne Oktoba 17 2023

Joel JJ By Joel JJ
17 Oct 2023
Tetesi za soka Ulaya, Jumanne Oktoba 17 2023

Kocha wa Roma Jose Mourinho anatarajiwa kuondoka katika klabu hiyo ya Italia mkataba wake utakapokalizika mwishoni mwa msimu huu, hakuna mazungumzo yoyote kuhusu yaliyofanywa kuhusu kuongezwa kwa mkataba wake. (Sky Sports Italia, kupitia Football Italia)

Kocha wa zamani wa Juventus, Chelsea na Tottenham Antonio Conte anasema siku moja angevutiwa kuinoa Roma au Napoli, na kwamba alikataa timu ya taifa ya Saudi Arabia. (Il Corriere della Sera, kupitia Football Italia)

Juventus wanaendelea kumfuatilia kiungo wa kati wa Denmark Pierre-Emile Hojberg, 28

Manchester United wanapania kumnunua beki wa Crystal Palace na Uingereza Marc Guehi, 23, ambaye amekuwa akihusishwa na llabu kadhaa za Ligi ya Premia. (Football Insider)

Aston Villa wanafikiria kumpa Leon Bailey kandarasi mpya, huku mkataba wa sasa wa winga huyo wa Jamaica mwenye umri wa miaka 26 ukikamilika Juni 2025. (Football Insider)

Arsenal wana uhakika wa kukubaliana mkataba mpya na beki wa Uingereza Ben White, 26, ambaye ana furaha katika klabu hiyo. (Fabrizio Romano)

Everton wanavutiwa na winga wa Corinthians wa Brazil Wesley Gassova, 18 - lakini watakabiliwa na ushindani. (Teamtalk)

Beki wa kati wa Ujerumani Malick Thiaw, 22, anataka kusalia AC Milan licha ya kutakiwa na Real Madrid na West Ham. (Calcio Mercato)

Borussia Monchengladbach wataanzisha kipengele cha kuongeza mkataba wa kiungo Mfaransa Manu Kone mwenye umri wa miaka 21 kwa mwaka mmoja ili uendelee hadi 2026. (Rheinische Post, via Get German Football News)

Kiungo wa kati wa Ubelgiji Romeo Lavia, 19, ambaye bado hajacheza mechi yake ya kwanza Chelsea tangu ajiunge nayo kutoka Southampton msimu wa joto, anatarajiwa kuwa nje ya uwanja hadi mwisho wa Novemba kutokana na jeraha la kifundo cha mguu alilolipata akiwa mazoezini. (Mail)

BBC

More Stories

Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe
Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe
37m ago
READ MORE →
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
2h ago
READ MORE →
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
2h ago
READ MORE →
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
4h ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
4h ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
4h ago
READ MORE →
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
4h ago
READ MORE →
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
4h ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
6h ago
READ MORE →
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
16h ago
READ MORE →