Awamu ya kwanza ya maboresho ya uwanja wa Benjamin Mkapa iko mbioni kukamilika kuelekea ufunguzi wa michuano ya African Football League utakaofanyika siku ya Ijumaa, Oktoba 20
Simba wenyeji wa michuano hiyo wataumana na Al Ahly katika mchezo ambao unatarajiwa kufuatiliwa dunia nzima
Wakati zoezi la kubadilisha viti likitarajiwa kufanyiwa baada ya AFL, kuna maboresho makubwa yamefanyika uwanjani kuanzia eneo la kuchezea 'pitch' na mabenchi ya ufundi
Leo zoezi la kufunga viti vipya kwenye mabenchi ya ufundi lilifanyika. Eneo la kuzunguuka uwanja pia yamefungwa mabango ya kidigitali ambayo yataanza kutumika rasmi siku ya Ijumaa







