Azam - Local

Bangala aumia tena kuikosa Yanga

Joel JJ By Joel JJ
β€’
18 Oct 2023
Bangala aumia tena kuikosa Yanga

Kiungo Yannick Bangala ameondolewa katika mipango ya Azam Fc kuelekea mchezo wa mzunguuko wa sita wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Young Afrcans

Miamba hiyo ya jiji la Dar es salaam itakutana Jumapili (Oktoba 22) katika Uwanja wa Azam Complex Chamazi

Kiungo huyo huyo aliyejiunga na Azam FC akitokea Young Africans, anaikosa Dar Dabi ya pili tangu ajiunge na timu hiyo, nyingine ilikuwa ile ya Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga

Ofisa Habari wa timu hiyo, Hashim Ibwe amesema kuwa mbali na kiungo huyo pia kuna na beki wa kati, Abdallah Kheir ‘Sebo’ ambaye alifanyiwa oparesheni ya goti

Ameongeza kuwa benchi la ufundi na uongozi wa timu hiyo, wanafurahia kurejea kwa mshambuliaji wao Mzimbabwe, Prince Dube aliyepona majeraha yake ambaye hivi sasa anaongezewa mechi fitinesi ili awe fiti kwa mchezo huo

"Bangala na Sebo ndio wachezaji pekee watakaokosekana katika mchezo wa Dar es salaam dabi tutakaocheza dhidi ya Young Africans, lakini wachezaji wengine wote wapo fiti"

"Bangala alipata maumivu ya misuli katika mchezo wetu wa ligi dhidi ya Dodoma Jiji, lakini hivi sasa anaendelea vizuri na upo uwezekano mkubwa wa kurejea haraka uwanjani baada ya kupata nafuu"

"Mchezo wetu huu ni muhimu kupata ushindi, kwa lengo la kulipa kisasi cha kufungwa katika nusu fainali ya Ngao ya Jamii, uzuri wachezaji wapo katika morali kubwa ya ushindi," amesema Ibwe

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
6h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
6h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
7h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
10h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
14h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
14h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
15h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
16h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
16h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
17h ago
READ MORE β†’