Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Alhamisi Oktoba 19 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
19 Oct 2023
Tetesi za soka Ulaya, Alhamisi Oktoba 19 2023

Liverpool wameungana na Chelsea na Arsenal katika kinyang'anyiro cha kumsaka mshambuliaji wa Napoli na Nigeria Victor Osimhen, 24, ambaye anakadiriwa kuwa pauni milioni 95. (Sun)

Mshambulizi wa Argentina Lionel Messi, 36, amepuuza tetesi kwamba ataondoka Inter Miami kwa mkopo kwenda kuchezea klabu nyingine mara tu msimu wa MLS utakapomalizika. (ESPN)

Inter Miami wanatarajia kumleta mshambuliaji wa Uruguay na Gremio Luis Suarez, 36, kwenye klabu ili kuungana na mchezaji mwenza wa zamani wa Barcelona Messi. (Mirror)

Mlinzi wa Chelsea Mbrazil Thiago Silva, 39, amedokeza kurejea Fluminense mwaka ujao, huku mkataba wake na The Blues ukitarajiwa kukamilika msimu huu wa joto. (Sun)

Bayern Munich wanapania kumnunua mlinzi wa zamani wa Arsenal Mgiriki Sokratis Papastathopoulos, 35, huku wakijaribu kupunguza athari ya majeraha yanayowakabili wachezaji. (Mirror)

Borussia Monchengladbach wameanzisha chaguo la kuongeza kandarasi ya kiungo wa kati wa Ufaransa Manu Kone huku Liverpool, Juventus na Bayern Munich wakimtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22. (90 min)

Newcastle wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Bayer Leverkusen na Nigeria Victor Boniface, 22. (Sun)

Bayern Munich wana uhakika wa kumsainisha kiungo wa kati wa Ujerumani Jamal Musiala kwenye mkataba mpya huku Liverpool na Manchester City zikiwa na nia ya kumsajili ingawa kandarasi ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 inaendelea hadi 2026. (90 min)

Nyota wa zamani wa West Ham Muitaliano Paolo di Canio, 55, amefichua kuwa alikataa nafasi ya kujiunga na safu ya ukufunzi ya Roberto Mancini katika timu ya taifa ya Saudi Arabia. (La Stampa, via Sun)

Rangers wamemwendea mkuu wa uajiri wa Brighton Sam Jewell, ambaye yuko nyuma ya wachezaji wakubwa waliosajiliwa na Seagulls. (Star)

BBC

More Stories

Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
1h ago
READ MORE β†’
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
11h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
11h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
12h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
15h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
19h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
19h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
20h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
21h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
21h ago
READ MORE β†’