Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Ijumaa Oktoba 20 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
20 Oct 2023
Tetesi za soka Ulaya, Ijumaa Oktoba 20 2023

Kocha wa Roma Jose Mourinho yuko tayari kurejea Real Madrid msimu huu, akichukua nafasi ya kocha wa sasa wa Los Blancos Carlo Ancelotti ambaye anatarajiwa kuchukua nafasi ya kocha mkuu wa Brazil. (Mundo Deportivo - kwa Kihispania)

Winga wa Manchester United Jadon Sancho ataorodheshwa kwa uhamisho mpaka aomuombe radhi kocha Erik ten Hag. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 aliachwa nje ya mechi ya United dhidi ya Arsenal mwezi uliopita kwa kutokidhi viwango vya mazoezi. (Guardian)

Liverpool wanaogopa kumnunua kiungo wa kati Jamal Musiala mwenye umri wa miaka 20 ingawa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 hana furaha kwa kuwa hana uhakika wa kuwa katika kikosi cha kwanza cha Bayern Munich. (Mirror)

Mkufunzi wa Newcastle United Eddie Howe hataki kuwa meneja ajaye wa England licha ya Chama cha Soka kumjumuisha kwenye orodha fupi ya watu wanaotarajiwa kuchukua nafasi ya Gareth Southgate. (Telegraph)

Chelsea wanatazamiwa kutekeleza chaguo la kuongeza mkataba wa Ian Maatsen, 21, hadi majira ya joto 2025 huku The Blues wakitumai watafanikiwa kumzuia beki huyo kujiunga na Barcelona. (Evening Standard)

Rais wa Barcelona Joan Laporta amekataa kumsajili Lionel Messi, 36, kutoka Inter Miami mwezi Januari, baada ya kujaribu kumrejesha Muargentina huyo Camp Nou msimu uliopita. (Fabrizio Romano kwenye X)

Lakini mkurugenzi wa michezo wa Barcelona Deco bado anasisitiza kuwa Messi hatimaye atarejea katika klabu yake ya zamani. (Sun)

Klabu ya Al Ettifaq ya Saudi Arabia iko tayari kumsajili mchezaji huru Jesse Lingard. Kiungo huyo wa zamani wa Manchester United mwenye umri wa miaka 30, ambaye anafanya mazoezi na kikosi cha Steven Gerrard, amekuwa bila klabu tangu alipoondoka Nottingham Forest msimu huu. (ESPN)

Manchester United itaongeza mkataba wa mwaka mmoja kwa mabeki Aaron Wan-Bissaka na Victor Lindelof na kusaini mkataba mpya na kiungo Hannibal Mejbri. (Manchester Evening News)

BBC

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
6h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
6h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
7h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
10h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
14h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
14h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
15h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
16h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
16h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
17h ago
READ MORE β†’