Mchezo wa mkondo wa kwanza African Football League kati ya Simba dhidi ya Al Ahly umemalizika uwanja wa Benjamin Mkapa kwa matokeo ya sare ya mabao 2-2
Ulikuwa mchezo wa vipindi viwili kwa Simba, kipindi cha kwanza timu ikicheza taratibu lakini ikaongeza kasi kwenye kipindi cha pili na kufanikiwa kufunga mabao mawili
Al Ahly walitangulia kufunga bao kwenye kipindi cha kwanza kupitia shambulizi la kushitukiza likifungwa na Slim
Kuingia kwa Sadio Kanoute na Jean Baleke katika kipindi cha pili kuliongeza uhai kwenye safu ya ushambuliaji na alikuwa Kibu Denis aliyerejesha Simba mchezoni kwa bao la kichwa akimalizia pasi ya Clatous Chama
Dakika sita baadae Kanoute akaongeza la pili kwa kichwa baada ya mpira wa kona kutoka kwa Saido
Kharaba akaifungia Al Ahly bao la pili baada ya shambulizi nyingine la kushitukiza wakati wachezaji wa Simba wakibishana mwamuzi Al Ahly wakaanza mpira haraka
Ilikuwa mechi ngumu iliyokutanisha timu bora, sare yanaweza kuwa matokeo rafiki kwa kila timu
Simba sasa inahitaji kujiandaa na mchezo wa marudiano ambao utapigwa Oktoba 24 huko Misri
Simba itahitaji kushinda mchezo wa pili au sare ya kuanzia mabao matatu ili kuweza kutinga nusu fainali

