Simba - Local

Al Ahly vs Simba kinapigwa Misri leo

Joel JJ By Joel JJ
β€’
24 Oct 2023
Al Ahly vs Simba kinapigwa Misri leo

Kikosi cha Simba kiko nchini Misri ambapo leo Wekundu hao wa Msimbazi wanakabiliwa na mchezo muhimu wa kuwania tiketi ya kutinga nusu fainali African Football League dhidi ya Al Ahly

Mchezo huo utapigwa saa 11 jioni katika uwanja wa Kimataifa wa Cairo

Hii ni mechi ya kuamua hatma ya tmu inayokwenda nusu fainali baada ya mchezo wa mkondo wa kwanza ulopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa kumalizika kwa matokeo ya sare ya mabao 2-2

Haijawahi kuwa rahisi kwa timu yoyote kupata ushindi dhidi ya Al Ahly wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani lakini timu kubwa zina tabia ya kupata matokeo mazuri katika uwanja wowote

Kwa hatua ambayo Simba imefika, hakuna hofu ya kucheza na yeyote iwe nyumbani au ugenini

Msimu uliopita kila mmoja anakumbuka kiwango bora walichoonyesha Simba kule Morocco kwenye robo fainali ya ligi ya mabingwa dhidi ya Wydad Athletic, ilikosekana bahati tu kwenye changamoto ya mikwaju ya penati

Ni mechi ambayo Simba inahitaji matokeo ya aina mbili tu, ushindi au sare ya kuanzia 3-3 ili kutinga nusu fainali. Kama timu hizo zitatoka sare ya mabao 2-2, changamoto ya penati itatumika kumpaka mshindi. Bado CAF wameweka msimamo katika bao la ugenini katika mashindano yao

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
2h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
2h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
3h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
4h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
5h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
19h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
20h ago
READ MORE β†’