Baada ya kipigo cha mabao 3-2 kutoka kwa Yanga, matajiri wa jiji la Dar es salaam Azam Fc wamerejea mazoezini kujiandaa na mchezo unaofuta kwenye ligi kuu dhidi ya Namungo Fc
Ijumaa saa 2:30 usiku Azam Fc itakuwa nyumbani uwanja wa Azam Complex kumenyana na Namungo ambayo hivi karibuni iliachana na kocha wake mkuu Cedric Kaze kutokana na mfululizo wa matokeo mabaya
Afisa Habari wa Azam Fc Hashehem Ibwe amesema wamesahau matokeo ya mchezo uliopita, focus yao ni kushinda mchezo dhidi ya Namungo
Ibwe amesema msimu huu wanataka kuwa mabingwa na Tanzania Bara hivyo ni wanachohitaji ni alama tatu ili kuendelea kubaki katika ushindani
"Tumepoteza mchezo dhidi ya Yanga, sio matokeo tuliyohitaji lakini ndio mpira wa miguu. Tumerejea mazoezini kujiandaa na mchezo unaofuata dhidi ya Namungo Fc"
"Malengo yetu hayajabadilika, tunautaka ubingwa wa ligi kuu msimu huu, Ijumaa tumejiandaa kuhakikisha tunapata alama zote tatu kwenye uwanja wetu wa nyumbani," alisema Ibwe
Baada ya kipigo cha Yanga, Azam Fc imeshuka nafasi ya tatu ikiwa na alama 13, alama mbili nyuma ya Simba inayoshika nafasi ya pili ikiwa na alama 15, Simba ikiwa na mchezo mmoja mkononi
Yanga ndio vinara wa ligi kuu wakiwa na alama 15 sawa na Simba lakini wana uwiano mzuri wa mabao



