Jana Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe alikumbana na wakati mgumu baada ya kutaka kushambuliwa na wanaodaiwa kuwa wasambazaji wa jezi feki za klabu ya Yanga na Simba
Tukio hilo liilotokea Temeke katika godown lililobainika kuhifadhi shehena ya jezi hizo feki zenye thamani ya Tsh Bilioni 10
Kamwe aliambatana na Waandishi wa habari kuwafichua wezi hao huku akiitaka Serikali iingilie kati kwani watu hao sio tu wanayima mapato klabu pia hawalipi ushuru wa Serikali
Wakati Ally alipofika eneo la tukio mlinzi wa eneo hilo alianza kuleta vitisha vya kutaka kumpiga kabla ya baadhi ya watu kumzuia
Tukio hilo lilirekodiwa 'mbashara' na kuwafanya watuhumiwa hao ambao walikuwa kwenye jitihada za kuhamisha shehena hiyo kushindwa
Ni wazi vita hii ni kubwa na inahitaji sapoti kubwa ya vyombo vya Serikali likiwemo Jeshi la Polisi
Meneja wetu wa Habari na Mawasiliano @AliKamwe akizungumza na waandishi wa Habari baada ya kukamatwa mzigo wa jezi feki jijini Dar Es Salaam.
— Young Africans SC (@YoungAfricansSC) October 25, 2023
Ally Kamwe ameiomba Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuzisaidia Klabu za Tanzania kupambana na watu wanaoingiza jezi feki… pic.twitter.com/CI8NQKD6lq



